Zitto Kabwe asema maisha yake yako hatarini
Huwezi kusikiliza tena

Mjadala mkali kuhusu mkaguzi mkuu na fedha trilioni moja nukta tano

Wakati mjadala mkali ukiendelea nchini Tanzania kati ya serikali ya nchi hiyo na kiongozi wa chama cha upinzani ACT Wazalendo Zitto Kabwe, kuhusu ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali na kuhusu kiasi cha fedha trilioni moja nukta tano,

hivi sasa mbunge huyo wa Kigoma ameiambia BBC kwamba maisha yake yapo hatarini.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Aboubakar Famau awali amefanya mahojiano na mwanasiasa huyo, na pia alitaka kujua ni kitu gani ambacho anahisi kimemweka hatarini.