Mafunzo maalum yanatolewa kuleta uwiano kati ya wafungwa na askari jela Kenya

Mafunzo maalum yanatolewa kuleta uwiano kati ya wafungwa na askari jela Kenya

Katika magereza mengi kote duniani, uhusiano kati ya Askari Magereza na wafungwa ni wa uhasama kama ule wa Paka na Panya.

Lakini mwandishi wa BBC Mercy Juma alipotembelea Gereza la Naivasha nchini Kenya alikuta mambo ni tofauti.

Huko mafunzo maalum yanatolewa ili kuyaleta pamoja makundi haya mawili na hivyo wafungwa na Askari Jela wanaishi kwa amani.