Uganda yaomboleza kifo cha Sokwe mkubwa zaidi nchini

Mbali na kuhifadhiwa, Sokwe huwa bado wanakuwa hatarini Haki miliki ya picha Terence Fuh Neba, WWF Central African Republic
Image caption Mbali na kuhifadhiwa, Sokwe huwa bado wanakuwa hatarini

Ijumaa kutakuwa na mkesha kuomboelza kifo cha Sokwe mkubwa zaidi nchini Uganda ambaye amekufa akiwa na miaka 54

Mwaka 1964, zakayo alikuwa na mwaka mmoja alipokutwa ametelekezwa magharibi mwa Uganda.Kituo cha elimu ya Hifadhi ya wanyamapori kimesema kuwa alitunzwa na wataalam na baadae alifikishwa kwenye hifadhi ya taifa akiwa na miaka 13.

Zakayo aliishi sehemu kubwa ya maisha yake katika hifadhi ya Entebbe, ingawa hapo kwa mujibu wa mamlaka nchini humo, alikuwa hatarini.Watalii walikuwa wanampa sigara na pombe ili awafurahishe.

Hifadhi hiyo kwa sasa imeboreshwa na Zakayo anayeitwa 'Babu' wa Sokwe wote nchini Uganda aliweza kuishi kwa raha

Wataalam wa uhifadhi wamemsifu Zakayo kwa kuwa balozi wa sokwe na wanyama wengine nchini Uganda.Wanasema wasifu wake ulisaidia kujipatia fedha kwa juhudi za uhifadhi na kuongeza idadi ya watalii

Mabaki ya Zakayo yatatunzwa kwa ajili ya utafiti na elimu.

Sokwe barani Afrika

Maisha ya Sokwe katika misitu barani Afrika hutegemea miti.

wanasayansi wameeleza hayo kutokana na utafiti walioufanya

utafiti ulibaini kuwepo kwa sokwe wengi kuliko wanyama wengine.

Haki miliki ya picha Emma Stokes/WCS
Image caption Sokwe katika nchi ya Cameroon,Afrika ya kati na Congo wanakabiliwa na tishio la ujangili

Hata hivyo , wanyama hao wengi wako kwenye maeneo yasiyo na usalama,ambapo huwa hatarini kuuawa na majangili,Ebola na uharibifu wa mazingira

Hali hiyo pia imewakuta sokwe wa kwenye misitu ya nchini Cameroon,Afrika ya kati ,Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Guinea ya Ikweta na Gabon.

Silaha inamaanisha uwindaji: vijidudu inaamisha Ebola:na miti inaashiria kuwa wanyama wanahitaji msitu kuweza kuishi,amesema Dokta Fiona Maisels,Mwanasayansi wa hifadhi kutoka taasisi ya hifadhi ya wanyama.

Ikiwa misitu itakatwa.Ikiwa misitu itabadilishwa na kuwa kwa ajili ya kilimo, hakutakuwa na sokwe.

Kwa mujibu wa jarida la kisayansi, Watafiti wa kimataifa wanasema viumbe wa aina hii wanahitaji uangalizi zaidi ya wanaoupata.

Jitihada za uhifadhi lazima zizingatie kuimarisha hatua za kupiga vita ujangili, hatua za kudhibiti magonjwa na kutunza mazingira, wameeleza.

Sokwe mzee zaidi kwenye hifadhi afariki Marekani

Sokwe mvuta sigara awasili Kenya