Mwanamke aliyetumia mtandao wa YouTube kujifungua

Tia baada ya kujifungua Haki miliki ya picha TIA FREEMAN
Image caption Tia baada ya kujifungua

Mama mmoja anasema kuwa alitumia kanda za video za YouTube kujifungua mwanawe baada ya kushikwa na uchungu ndani ya chumba cha hoteli akiwa pekee.

Tia Freeman, kutoka Nashville aliambia Newsbeat kwamba alidhania kwamba uchungu wa uzazi ulikuwa sumu. Tia na mwanawe wa kiume wako salama.

Ilianza na kipimo cha kubaini mimba, safari ya kuelekea Ujerumani na kupumzika nchini Uturuki.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 anasema kuwa hakujua kwamba amebeba uja uzito hadi mwisho wa mimba hiyo.

Niligundua katikati ya mwezi Januari, aliambia Newbeat. Niliongeza kilo tano pekee katika kipindi chote cha uja uzito , hivyobasi kuongeza uzito huo hakukunitia wasiwasi. Alidhani kwamba uzani huo ulikuwa wa kawaida , akidhania ni kutokana na kwamba hakuwa akienda kwa mazoezi.

Lakini mara mimba hiyo ikaanza kukuwa na hatua iliomfanya kuchukua kipimo.

Licha ya kugundua kuhusu habari hizo , Tia anadai kwamba hakuamini na hivyobasi akaamua kutomwambia mtu yeyote. Badala yake alielekea ziarani Ujerumani akiamini akijua kwamba hakutakuwa na tatizo lolote iwapo angejifungua.

Lakini mambo yalibadilika alipoanza kuhisi uchungu wakati wa safari hiyo ya saa 14. Tia alidhani kwamba chakula kilikuwa na sumu lakini wakati alipowasili Uturuki ,taifa alilopumzika alikuwa akitokwa na jasho na kuhisi kana kwamba alitaka kutapika.

Ni wakati huo ambapo aligundua kwamba alikuwa ameshikwa na uchungu, baada ya kutazama katika mtandao wa Google.

Alipowasili katika hoteli yake bila kujua cha kufanya , Tia hakutumia njia ya kawaida ya kutaka usaidizi wa kimatibabu. badala yake aliamua kuingia katika YouTube , na kutuma ujumbe katika twitter.

Tia anasema kuwa alijaza beseni la kuoga kwa maji moto , akachukua taweli kabla ya kutafuta njia nzuri za kujifungua katika mtandao.

Wakati alipoanza kujifungua, Tia anasema kuwa uchungu wake ulikuwa ukija baada ya dakika moja .Huku akituma ujumbe wa twitter kwamba hajawahi kuhisi uchungu wowote kama huo katika maisha yake, pia alisema kwamba alijifungua mwanawe kwa haraka sana.

Licha ya kushangaa, Tia anasema kwamba hakuogopa-anasema kwamba alitumia mtandao kutoa kondo la nyuma. Na baadaye akatumia kamba zake za viatu kufunga kitovu.

Wakati aliporudi katika uwanja wa ndge ili kurudi nyumbani siku iliofuata na mwanawe mchanga alisema kuwa wafanyikazi wa uwanja huo wa ndege waliogopa.

Haki miliki ya picha TIA FREEMAN
Image caption Mwana wa Tia Xavier

Walidhani nilikuwa mlanguzi wa binaadamu ambaye najaribu kusafirisha mtoto.

Baada ya kuwaelezea kwamba hakumuiba mtoto huyo na kwamba ni wake, Tian anasema kwamba Kampuni ya ndege ya Turkish Airline ilimlipia hoteli kwa wiki mbili mjini Istanbul ambapo alikuwa akiangaliwa na maafisa wa matibabu.

Mada zinazohusiana