Korea Kaskazini kufunga eneo la kufanyia majaribio ya nyuklia Mei

This DigitalGlobe satellite image of the Punggye-ri Nuclear Test Facility in North Korea was taken February 11, 2013. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption A satellite image of the Punggye-ri nuclear test site in North Korea

Korea Kusini imesema kuwa Korea Kaskazini imeahidi kufunga eneo lake la kufanyia majaribio ya nyuklia mwezi ujao na itaalika wataalamu wa kimataifa na waandishi wa habari kushuhudia kufungwa eneo hilo.

Ofisi wa ya rais nchini Korea Kusini imesema kuwa pia Korea Kaskazini imekubali kubadilisha saa zake kuwa sawa na za Korea Kusini, ikiwa ni ishata nzuri kwa kuwa kwa sasa saa ya Korea Kaskazini iko nusu saa nyuma ya ile ya Korea Kusini

Korea Kusini inasema hatua hizo zinakuja baada ya mkutano wa kihistoria wa siku ya Ijumaa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

Pyongyang awali ilikuwa imetangaza kuwa eneo hilo la kufanyia majaribio lingefungwa.

Iliripotiwa kukana madai ya wanasayansi wa China kuwa eneo hilo lilikuwa limeharibiwa vibaya na halingeweza kutumiwa tena.

Siku ya Ijumaa, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in walikutana kufanya kazi wakiwa pamoja kuondoa zanaza nyuklia rasi ya Korea,

Mkutano huo ulfanyika miezi michache babda ya matamshi ya kivita kutoka Korea Kaskazini.

Mada zinazohusiana