Vijana wana mchango gani kwa uchumi wa Nigeria

Wafanya biashara nchini Nigeria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafanya biashara nchini Nigeria

Rais wa Jamuhuri ya Nigeria, Rais Muhammadu Buhari alieleza kuwa vijana wengi ni wavivu mbele ya mkutano wa kimataifa wa kibiashara jambo ambalo liliwakwaza wengi

Raia wengi wa Nigeria walikuwa wakifuatilia kauli ya rais wao,Muhammadu Buhari alipotembelea London juma lililopita

Akizungumza wakati ya jukwaa la biashara la jumuia ya madola, rais Buhari alisema Vijana 'wengi' wa Nigeria ''hawafanyi chochote'' lakini wanategemea kuwa na nyumba nzuri, huduma nzuri za afya na elimu bure''.

Bila kutarajia mitandao ya kijamii iliibuka na Hashtag iliyopewa jina #LazyNigerianYouths (vijana wavivu wa Nigeria)

katika taarifa yake aliyoitoa baadae, rais aliitetea kauli yake.Vyombo vya habari vya serikali vilieleza kuwa rais hakutumia neno ''wavivu'', lakini utetezi huo haukusaidia kushusha hasira za raia kwenye mitandao.

Maelezo ya mmoja wapo wa watumiaji wa mtandao wa Twitter aliandika '' Nina miaka 22 nina ufaulu wa daraja la pili kwenye masomo ya Sayansi ya Kemia ya Chuo kikuu cha Lagos,Sasa ninatengeneza viatu kwa sababu sikuweza kuajiriwa, mimi si mvivu,mimi si mvivu, mimi si mvivu #LazyNigerianYouths".

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Buhari alikutana na Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May katika wiki ya mkutano wa jumuia ya madola

Je vijana wanachangia kiasi gani katika uchumi wa Nigeria?

Kama rais Buhari alivyosema kwenye hotuba yake, asilimia 60 ya raia wake wana umri wa chini ya umri wa miaka 30, kwa makisio ni takriban watu milioni 107.

wengi wao bado watoto lakini wengi wako kwenye umri wa kufanya kazi lakini bado hawapati kazi.

tatizo la ukosefu wa ajira nchini Nigeria limeongezeka mara tau tangu mwaka 2014 mpaka 2017 kutoka asilimia 6.4 mpaka 18, kwa mujibu wa taasisi ya taifa ya takwimu.

Wakati huo huo, uchumi wa Nigeria, ambao unategemea usafirishaji wa mafuta nje ulishuka kwa sababu ya kuporomoka kwa bei ya mafuta duniani, ingeeleweka kuwa vijana wangetafuta kazi

Ingawa kulikuwa na mdororo wa uchumi, katika makundi yote ya umri , idadi ya watu waliotafuta kazi iliongezeka kwatakriban watu milioni moja.(Mdororo wa uchumi uliisha mwezi Septemba mwaka 2017)

Pamoja na kutokuwa na uzoefu katika soko linaloendelea kuwa na ushindani kila siku, kama ilivyo kwa wazee, vijana walikuwa tayari kuzing'ang'ania kazi zao na hata kutafuta kazi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vijana wengi wanafanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi

Katika Ripoti ya watafiti wa kiuchumi kutoka Chuo cha Berkley mjini California, imesema kuwa raia wa Nigeria walitumia zaidi ya wanachokipata mpaka walipotimiza miaka 32. hiyo inamaanisha kuwa ,pamoja na kufanya kazi, hawakupata faida ya kutosha.

Changamoto hii ilikuwa miaka 14 iliyopita , hatujui kama hali iko hivi hata sasa.Lakini kumekuwa na hali ya kupanda kwa gharama za maisha kwa kipindi cha miaka mitatu, ni hivi karibuni tu bado mishahara haijapanda, hivyo inawezekana bado vijana wanakabiliwa na changamoto ileile wakiwategemea ndugu zao.

Shirika la fedha duniani, IMF limesema Vijana wengi nchini Nigeria wanafanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi, ambayo ndio kubwa zaidi lakini sekta hii ndio yenye watu wenye ujuzi mdogo, ujira mdogo, mazingira duni ya kazi na faida duni.