Sundowns wapania kunyakua kombe ligi ya mabingwa Afrika

Pitso Mosimane ameiongoza Mamelodi Sundowns kujinyakulia mataji matatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pitso Mosimane ameiongoza Mamelodi Sundowns kujinyakulia mataji matatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita

Mamelodi Sundowns sasa malengo yao wameyaelekeza kwenye ushindi wa kombe la ligi ya mabingwa Afrika baada ya kupata ushindi katika michuano ya ligi kuu nchini Afrika Kusini siku ya Jumamosi.

Sundowns wamejihakikishia ubingwa wa nchini kwao baada ya kupata ushindi wakitoka nyuma kwa kuifunga Ajax Cape Town kwa 3-1 katika mchezo uliochezwa Atteridgeville, Pretoria. timu hiyo alipata magoli ya ushindi kupitia kwa Mzimbabwe Khama Billiat, Ricardo Nascimento na Sibusiso Vilakazi.

Jumamosi ijayo mabigwa hao wa msimu wa 2016, wa michuano ya klabu bingwa Africa watashuka dimbani kuibali Wydad Casablanca ya nchini Morroco ,katika mchezo wa hatua ya makundi,

Mchezo huu ulikuwa pia wa kumuaga Khama Billiat, ambae anaondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa mwezi Mei na kujiunga na timu ya FC Qarabaq ya Azerbaijan.

Sundowns walikuwa wanaongoza kwa alama 4 mbele ya Orlando Pirates ambao wako nafasi ya pili, Timu hii ilihiutaji ushindi ili kutwaa ubingwa ligi kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka mitano chini ya kocha Pitso Mosimane.

Hata kama Mamelodi wangepoteza mchezo huo wangetwaa ubingwa kwa kuwa timu iliyokuwa na uwezo wa kuwafukuzia Orlando Pirates ilipoteza mchezo kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Cape Town City.

Tayari Mamelodi na Orlando wamejikatia tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.