Benedict: Nilikuwa ninaabudu shetani

Benedict alizaliwa kwenye familia iliyoshika sana dini ya kikristo Haki miliki ya picha Rebecca Hendin / Getty / BBC Three
Image caption Benedict alizaliwa kwenye familia iliyoshika sana dini ya kikristo

Nilianza kuingia kwenye dini ya mashetani nilipokuwa na miaka 15.

Wazazi wangu ni Wakristo walioshika imani sana na walikuwa wakituchukua mimi na dada yangu kwenda kanisani tulipokuwa wadogo, miaka michache baadae nilikuwa nikisikiliza aina ya miziki ambayo baadae ilinifanya niwe mlevi na mtumia madawa ya kulevya.

Ikawa ni swala la kuchagua, kutoka na marafiki ambako kulinifanya niuone ulimwengu au kusikiliza hadithi za biblia na wazazi wangu na kupaka rangi picha ya safina ya Noah, Nilichagua kuwa mtukutu.

Nilipenda mno muziki wa rock wakati huo, nilikuwa napiga gitaa kwenye bendi na baadhi ya marafiki, ilikuwa njia rahisi ya kutambulika, nilivaa nguo za bendi, na katika umri huo ujana unakufanya uwe na shauku ya kujaribu vitu, wakati mwingine nilikuwa najiremba ili kuwavutia wasichana.

Usiku mmoja nikaona Biblia ya shetani nyumbani kwa rafiki yangu, niliichukua kwenye rafu ya vitabu na nikaisoma mara moja. Iliandikwa na mwazilishi wa kanisa la shetani, Anton LaVey, nakala zaidi ya milioni moja tangu kilipochapishwa mara ya kwanza mwaka 1969.Kilinivutia.

Sikuwa na furaha kwenye mahusiano yangu na mpenzi wangu wa zamani na nilikuwa nabishana na wazazi wangu .

Siku iliyofuata, nilikuwa na mvutano na mama, nikajifungia chumbani na kuanza kuchora alama ya kanisa la shetani kwenye mkono wangu.Kulikuwa na damu nyingi, lakini haikunizuia, Nilitaka kujiweka michoro ya kudumu kwenye mwili wangu.

Watu wana tafsiri tofauti, kwangu dini ni kuhusu kujipenda mwenyewe, Wanaoamini ushetani wanaamini katika kufanya kila kitu kilicho kwenye uwezo wao kupata wanachokitaka maishani, kama vile ngono,chakula na pombe.

Inakufanya uwe mbinafsi kujipenda mwenyewe bila kujali wanaokuzunguka.

Haki miliki ya picha Rebecca Hendin / Getty / BBC Three
Image caption Benedict Atkins

Lakini kuna wakati, nikahisi kama Mungu wa Kikristo ambaye tangu mtoto nimekuwa nikimwabudu, ambaye ni mwema, haonyeshi kujali namna nilivyokuwa nikihangaika.

Nilikuwa najiumiza na ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.Ukristo haukunipa faraja yeyote, ilikuwa ni kujifanya kama vile kila kitu kilikuwa sawa.

Imani ya kishetani iliniingia hasa,yakawa maisha yangu.

Nilichora alama ya kanisa hilo kwenye kila kitu, kwenye vitabu vyangu vya shulr, mwilini mwangu.

Marafiki zangu na mpenzi wangu waliona sasa nitafika mbali kutokana na vitendo vyangu vibaya, nilitoka kuwa mtu maarufu kiasi na nuwa mtu nisiye na marafiki.

Siku moja nikaota shetani kasimama pembeni mwa kitanda changu, alikuwa amevaa vizuri, akizungumza vizuri kama vile muigizaji wa filamu ya Sherlock Holmes.Alisimama hapo na akasema unaenda kumaliza mitihani yako kisha utakufa.

Nikashtuka ''hii mbaya sana''.

baada ya muda nikaanza kupata ndoto mbaya na kugundua kuwa hali hiyo inanisumbua.Kuna wakati nilijiuliza, 'kweli ninazungumza na shetani?' uhusiano wangu na mpenzi wangu ulivunjika, nilikuwa nimeigeuka familia yangu na kupoteza marafiki zangu wengi.

Nilijihisi kutengwa na sikuwa na wa kumtegemea isipokuwa shetani.Nilimaliza mitihani, na nilikuwa hai bado.Mara,ilikuwa wazi kabisa kwangu nikaona kuwa shetani ni muongo.

Wokovu ulikuja bila kutegemea.

Rafiki wa Dada yangu ambaye alikuwa mtoto wa mchungaji, alinialika kwenye tamasha la kikristo. Lilikuwa tukio la wiki nzima.

Kwa kweli nilikwenda kwa sababu nilifikiri kuwa kutakuwa na wasichana wanaovutia. Lakini nilishangazwa kukuta kuwa kulikuwa na watu wengi ambao wako kama mimi, hawakuwa na furaha ndani ya ukristo.

Haki miliki ya picha Rebecca Hendin / Getty / BBC Three
Image caption Benedict Atkins aliyekuwa akiabudu shetani amerejea kwa Mungu

Usiku wa mwisho wa tamasha lile, nilikuwa nikisikiliza mazungumzo kuhusu namna ya kubaini kuwa umeanguka.Alipokuja mtu mmoja kuniombea, sikujua cha kusema hivyo nilikubali.

Wakati alipokuwa akiomba, nilijisikia amani ndani yangu, baadaye yule mtu akasema hata kama nilikuwa nikijisikia sina matumaini maishani, Mungu alikuwa na mpango na mimi na kuwa shetani ni muongo.

Nilikwenda nyumbani nikijisikia kuwa huru na mwenye mtazamo chanya kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi.Nikaanza kuutazama ukristo tena, lakini si kukubali tu bila kuhoji, kama nilivyokuwa nikiiambiwa kufanya kabla.

Nilianza kuongozana na watu wachache ninaokutana nao kanisani kwa wazazi, kama mimi hawakupendakukaa chini tu na kusikiliza mahubiri.

Ngono, dawa za kulevya na muziki wa rock n roll zilikuwa burudani zangu tangu nikiwa mdogo, ilinichukua miaka kadhaa kujua kuwa haina haja ya kutumia hivyo ili kujisikia vizuri.

Nikaanza kwenda kanisani mara kwa mara na nikajihisi kuwa na mimi ni mmmoja wao.

Nilipofikisha miaka 20, nilikutana na mke wangu, Sarah, kutokana na kanisa. Ndoa yetu sasa ina miaka mitatu.

Sikuwahi kufikiria kuwa Mchungaji, nilipata kazi Canning Town South London baada ya masomo ya chuo kikuu, nilifanya kazi na watoto wanaopata ugumu wa kuandika (dyslexic) kutoka kwenye magenge ya mitaani, wakati huohuo, nilijiunga na kanisa jingine katika eneo hilo na kujikuta nikiombwa ushauri na waumini wadogo kuhusu maswala ya kiroho.

Nikashangaa.. ''loh haya ni majukumu makubwa sana''.

Nikaamua kusoma sana na kujiunga na masomoya biblia nikasoma shahada ya kwanza ya masomo hayo katika chuo cha Nottingham.

Kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, nimekuwa mchungaji East London, sijioni kuwa mtu mwenye mamlaka, ni mtu tu wa kawaida.

Ninapofikiria jinsi nilivyojiona nimepotea na mwenye kuogopa wakati nilipokuwa na imani ya kishetani, inanifanya nipate moyo wa kusaidia watu.

Ndio maana ninafanya kazi hii.Jina langu Benedict, maana yake baraka-Nilizaliwa kutokana na uzazi uliokuwa mgumu ambao ulifanya maisha yangu na ya mama kuwa hatarini.

Katika siku zangu zenye giza, nilipoteza umaana wa kuwa baraka.Sasa nataka kuishi hapa Canning Town mpaka Mungu atakaponiamulia kuendelea kuishi au kufa.

Unaweza kusoma pia: