Mo Ibrahim: sekta za umma ni changamoto Afrika

Mwenyekiti wa Mfuko wa Mo Ibrahim, Mohammed Ibrahim
Image caption Mwenyekiti wa Mfuko wa Mo Ibrahim, Mohammed Ibrahim

Mwenyekiti wa mfuko wa Mo Ibrahim, alikutana na viongozi wa Afrika na wataalam ili kuzungumzia changamoto za Sekta za umma.

Aliwakutanisha wajumbe zaidi ya 1000 mjini Kigali Rwanda wakiwemo viongozi, wanasiasa,wafanya biashara wawakilishi wa asasi za kiraia na mashirika ya kimataifa, kujadili maswala kuhusu mustakabali wa Afrika.

Mwaka huu mkutano ulitilia mkazo maswala ya huduma za sekta za umma barani Afrika.

Huduma kutoka idara za umma zinakwenda sambamba na ukuaji na ongezeko la kasi ya watu barani?

Image caption Maelfu ya wagonjwa huishia kuhangaika katika hospitali za umma kila kunapokuwa na migomo ya kitaifa ya madaktari na wahudumu wa afya wanaotaka malipo zaidi.

Changamoto za utoaji wa huduma kwenye sekta za umma

Mfuko huu unatazama maswala ya utawala, kwa mujibu wa Mo Ibrahim, utawala ni kuhusu pia utoaji wa huduma kwa umma, lakini ni nani anapaswa kutoa huduma hizo? ameuliza .

Sekta ya huduma kwa umma ni muhimu , kwa bahati mbaya waafrika hawalitilii uzito unaostahili, mfuko wa Mo Ibrahim unaona swala hili halipewi kipaumbele vya kutosha.

Nchi nyingi za Afrika hazina uwezo mkubwa wa kukidhi mahitaji na kuweza kutoa huduma ipasavyo kutokana na changamoto za kifedha.

Wachambuzi wa mambo wanasema viongozi wana nafasi kubwa kuhakikisha kuwa wanazipeleka nchi mbele kwa kuboresha mazingira ya huduma kwa umma kama vile maswala ya miundo mbinu, kuboresha maisha ya watu wake, kuboresha miundombinu kama vile ya afya na elimu.

Huwezi kusikiliza tena
Uwiano wa idadi ya walimu na wanafunzi unaathiri masomo Tanzania?

Mfano nchini Tanzania, huduma za sekta za umma zimekuwa zikinyooshewa vidole tofauti na sekta binafsi , kwa mfano katika maswala ya elimu.

Nchini Tanzania, idadi kubwa ya waalimu imekuwa njia panda hasa kutokana na kipato duni wanachopokea kila mwezi, kumekuwa na mazingira duni ya ufundishaji, kukosa vifaa vya kufundishia, msongamano wa wanafunzi na upungufu wa madawati.

Hali hii inajitokeza kutokana na kukosa fedha za kutosha ili kuboresha sekta ya elimu nchini.

''Hili linataka utashi wa kisiasa, sekta ya elimu inahitaji uwekezaji mkubwa sana, kwa mfano mwaka huu wa fedha , fedha iliyotengwa kwenye elimu ni asilimia 15 ya bajeti hivyo malengo ya makubaliano ya kimataifa kuhusu elimu itakuwa vigumu kufikia''.Ameeleza mtaalamu Godfrey Boniventura kutoka taasisi ya utafiti ya Haki elimu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii