Kwa nini unafaa kubadilisha nywila yako ya twitter leo

Twitter logo Haki miliki ya picha Getty Images

Kampuni ya mtandao wa Twitter imewaonya watumiaji wake milioni 330 kubadilisha nywila zao baada ya tatizo kufanya maneno hayo ya siri kuonekana kwa maandishi.

Mtandao huo wa kijamii umesema kuwa uchunguzi umonyesha kuwa hakuna maneno ya siri yalioibwa. Hatahivyo umewataka watumiaji wake kubadilisha nywila zao kama hatua ya tahadhari.

Twiter haikusema ni nywila ngapi ziliathiriwa.

Inaeleweka kwamba idadi hiyo ilikuwa kubwa na kwamba zilionekana kwa miezi kadhaa. Afisa mkuu wa Twitter Jack Dorsey alituma ujumb wa twitter.

Tatizo hilo lilihusishwa na utumizi wake wa ambao unazifanya nywila kutumika kupitia nambari na herufi. Kuna proramu ambayo huzihifadhi katka logi ya komyuta kabla kutumika kupitia nmabri na herufi katika blogi yake.

Image caption watumiaji walipokea ujumbe uliowaonya wakati walipkuwa wakiingia katika akaunti zao

"Tunaomba msamaha kufuatia ugunduzi huo'', twitter ilisema katika blogi yake

Mbali na kubadilisha nywila , wateja wameshauriwa kuweka huduma za ulinzi ili kuzuia akaunti kudukuliwa.

Afisa mkuu wa teknolojia katika mtandao huo Parag Agrawal awali alikuwa amesema kuwa kampuni hiyo haikuwa na haja ya kufichua habari hiyo lakini inaamini ilikuwa kitu muhimu kufanya -kabla ya kusahihisha makosa yake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii