Tuzo ya Nobel ya fasihi yaahirishwa kwa sababu ya kashfa

Shule ya Sweden itatangaza mshindi wa mwaka 2018 na 2019 mwakani Haki miliki ya picha AlfredNobel.org
Image caption Shule ya Sweden itatangaza mshindi wa mwaka 2018 na 2019 mwakani

Taasisi inayotoa tuzo ya nobel ya fasihi imesema haitatoa tuzo hiyo mwaka huu, baada ya kukumbwa na shutuma za udhalilishaji wa kingono

Taasisi hiyo ya Sweden imekuwa kwenye mzozo mkali kutokana na namna wanavyoshughulikia shutuma dhidi ya mume wa mfanyakazi wa taasisi hiyo

Taasisi imesema itatangaza mshindi wa mwaka 2018 na mshindi wa mwaka 2019 mwakani.

Kashfa hii ni kubwa kukumba tuzo hiyo, tangu ilipoanza kutolewa mwaka 1901.

Mbali na miaka sita wakati wa vita vya dunia, ni mwaka mmoja pekee tuzo hiyo haikutolewa.Hakukuwa na mshindi mwaka 1935

Tuzo nyingine za Nobel zitafanyika kama kawaida.

Mgogoro ulianzaje?

Mgawanyiko ulianza kujitokeza mwezi Novemba mwaka jana baada ya mpiga picha raia wa Ufaransa Jean-Claude Arnault aliyekuwa akifanya kazi ya kuongoza mradi wa maswala ya tamaduni uliokuwa ukifadhiliwa na shule ya Sweden, alikuwa akishutumiwa kuwadhalilisha kingono wanawake 18.

Wanawake kadhaa kati yao waliripoti kuwa vitendo hivyo vilifanyika kwenye maeneo yanayomilikiwa na shule hiyo.Bwana Arnault amekana shutuma hizo.

Madai hayo na shutuma kuhusu mgongano wa maslahi na kuvuja kwa majina ya washindi wa tuzo ya Nobel pia ni sababu zilizoigawa taasisi hiyo.

Baada ya shutuma hizo kukatokea wimbi la wafanyakazi wake kuacha kazi, akiwemo mkuu wa shule hiyo, Profesa Sara Danius.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Profesa Sara Danius ni Mkuu wa Sweden Academy

Hizi ni Tuzo gani?

Mwanasayansi wa Sweden, Alfred Nobel alianzisha kwa mapenzi yake tuzo hizi mwaka 1895

Hutolewa tuzo tano, kwenye Kemia, fasihi andishi, tuzo ya amani,Fizikia na Fiziolojia(Dawa)

Tuzi ya Nobel ya uchumi ilifanyika mwaka 1968 kwa ajili ya kumkumbuka Alfred Nobel

Washindi wa Tuzo za Nobel

  • Tutu, Desmond Mpilu (Afrika Kusini) -Alipata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984: Ni mmoja kati ya wanaharakati wa haki za binaadam , alipata tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kumaliliza vitendo vya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini .Alikuwa Kiongozi wa kwanza mweusi wa madhehebu ya Anglikana wa mji wa Cape town na Johannesburg. Aliitwa sauti ya wasio na sauti, alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kibaguzi.Nelson Mandela alipokuwa Rais wa kwanza mweusi nchi humo, alimteua Tutu kuwa mwenyekiti wa tume ya ukweli na maridhiano.
  • Zewail, Ahmed Hassan (Misri)-Alipata tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka 1999 kuhusu mabadiliko ya kemikali.Zewail alikuwa mwanasayansi wa kwanza mwenye asili ya kiarabu kupata tuzo hiyo.
  • Johnson Sirleaf, Ellen (Liberia)-Alipata tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2011 kutokana na juhudi za kupambania usalama wa wanawake , haki za wanawake na ushiriki wa wanawake katika kazi ya kuijenga amani ya Liberia.Mwanamama huyu ni rais wa kwanza mwanamke barani Afrika aliyechaguliwa kidemokrasia,alichangia sana kuimarisha amani ya Liberia na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuimarisha nafasi za wanawake.
  • Wangari Maathai (Kenya)-Alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel , Mama Wangari aliweka jitihada zake katika kupigania haki za binaadamu na haki za wanawake .Pia alipigania utunzaji wa mazingira , si Kenya pekee bali Afrika alianzisha kampeni ya kupanda miti na kuwahamasisha wengine kuwajibika kutunza mazingira yao, serikali yao inayowaongoza, maisha yao na mustakabali wa maisha yao.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii