Hawaii yakumbwa na Kimbunga pamoja na volkano

Hawaii,volkano
Image caption Uji wa Volkano ukiruka juu

Kisiwa kikubwa cha Hawaii kimepigwa na kimbunga kinachotajwa kuwa kikali taangu mwaka 1975.

Kimbunga hicho cha kipimo cha ritcha 6.8 kimewafanya watu kuondoka majumbani mwao, pia kikiharibu miundombinu ya umeme na maji.

Kimbunga hicho kinatajwa kuanzia kwenye mlima wa volcano uitwao Kilauea. Kwa mujibu wa mashuhuda, tetemeko hilo liliambatana na upepo mkali ambao uliharibu vitu mbalimbali.

Mamia ya wakaazi wa eneo hilo tayari wametafuta hifadhi kutoka maeoe ambayo hayajaathirika.

Maija Stenback, shuhuda wa kimbunga hicho

Tunaishi eneo la mashambani Leilani, karibu vitalu sita vilisambaratishiwa mbali na mlipuko.tuliondolewa eneo hilo saa kadhaa zilizopita na sasa tumejihifadhi kwa marafikiu.

Nusu saa baada ya kimbunga hicho , nilishangaa kukuta mitandao mingi imeandika juu ya tukio hilo , kwa hiyo mimi na binti yangu tukatoka kwenda kujionea kwa macho yetu kwakweli unaweza kusikia na kuhisi mlipuko ukiwa umbali wa nusu maili na kadiri unavyokaribia eneo la tukio ndivyo unavyozidi kulihisi .Ilikuwa kama wakati mtu anavyopiga gitaa la besi kwakweli nzito, na unaweza kuhisi kweli nguvu ya uji wa volkano, rangi nayo sasa ilikuwa ya kustaajabisha na sauti ya volkano hiyo kwakweli ni maajabu makubwa .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Barabara zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na volkano hiyo

Unaweza kukadiria ukubwa wa mlipuko wa volkano hiyo kwa masikio yako mwenyewe , vokano ilikuwa inarusha uji wake mbali kadiri inavyoweza na huwezi kukadiria wazi nini unachokisikia bali kile unachohisi.

Pamoja na kitisho chote hicho wako baadhi ya watu wamegoma kuhama katika maazi yao.Kufuatia hali hiyo hali ya hatari imetangazwa katika eneo hilo na wakaazi wapatao 1,700 wamehamishwa kutoka eneo hilo.Vituo vya kijamii vimefunguliwa ili kutoa makazi kwa waathirikaKilauea ni mojawapo ya eneo lenye volkano yenye nguvu na mlipuko zaidi duniani kufuatia mfululizo wa matetemeko ya hivi karibuni.

Maafisa wa serikali wameendelea kutoa angalizo kwa wakaazi wa maeneo hayo na ya jirani kwamba kwa wiki ijayo yote wanapaswa kuwa katika tahadhari kubwa na mara wakihisi viashiria vya kutaka kulipuka kwa volkano haraka iwezekanavyo na hii ni kwa wale wote waliogoma kuyahama makaazi yao

ukanda wa volkano iliyojulikana kama Puu Oo - ulilipuka mapema wiki hii, na kuteremka chini ya mteremko wa mlima kuelekea maeneo ya makazi.

Gavana wa Hawaii , David Ige, alisema kuwa alikuwa ametoa ushawishi kwa wanajeshi na vikosi vya usalama wa taifa hilo kusaidia katika shughuli za uokozi wa maelfu ya watu.