Binti mfalme bado anasakwa

missing dubai princess
Image caption Mohammed bin Rashed al-Maktoum mfalme wa Dubai

Kikundi cha kutetea haki za binaadamu chenye kuongoza harakati za wapi alipo binti mfalme ,kimehimiza mamlaka za Dubai kufumbua fumbo la wapi alipo binti wa mtawala wa Emirate,Mohammed bin Rashed al-Maktoum.

Inaarifiwa kuwa binti mfalme aitwaye Latifa alikuwa katika jaribio la kutoroka kasri na nchi yake kwa lengo la kwenda kuishi maisha huria nje ya mipaka ya ufalme.

Ingawa mashuhuda wanadai kuwa boti ya kifahari aliyokuwa anasafiria ilivamiwa na maafisa wa kulinda usalama wa pwani katika bahari ya Hindi, na baada ya hapo walimkamata binti mfalme na kumrejesha Dubai, na tangu wakati huo hajulikani aliko.

Maafisa wa ufalme waliiambia BBC kuwa hawawezi kuzungumzia chochote juu ya sakata la binti mfalme kutokana na sababu za kisheria , na kuongeza kuwa wanaowashikilia walikuwa na historia ya shughuli za jinai.