Upandikizaji kwenye via vya uzazi ni hatari

Baadhi ya vipandikizi vimesababisha maumivu makali na hali ya kudhoofika
Image caption Baadhi ya vipandikizi vimesababisha maumivu makali na hali ya kudhoofika

Mwanamke mmoja ambaye amekuwa na maumivu kwa muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji na upandikizaji kwenye via vya uzazi ametaja upandikizaji huo kukomeshwa, huku wataalamu wakisema njia hiyo inatakiwa kuwa suluhu ya mwisho .

Serikali ya Wales imependekeza zifanyike njia nyingine za kutibu wagonjwa wenye shida kwenye via vya uzazi.

upandikizaji huo umedaiwa kusababisha maumivu makali na kuwafanya wagonjwa kuwa wadhoofu.

Jemima Williams amekuwa kwenye maumivu yasiyokwisha tangu alipofanyiwa upasuaji.

Upandikizaji maalum wa ngozi unauwezo wa kukabiliana na saratani

Mtu wa kwanza kupandikizwa uume duniani

Mamia ya wanawake wameripoti kuhusu upandikizaji kwenye via vya uzazi

Mwanamama ambaye alifanyiwa upandikizaji mwaka 2002 baada ya via vya uzazi kupoteza nguvu zake, anasema ''silali..ninaamka nikiwa na maumivu makali,maumivu kwenye uke,maumivu ya rektamu.

pia nina maumivu kwenye uti wa mgongo, na maumivu ya nyonga na maumivu hasa kwenye mguu wa kushoto kwenda chini.''

Bi Williams ambaye anapata tabu mara nyingi kuamka kitandani kutokana na shida anayopata baada ya kupandikizwa, amefanya upasuaji mara nyingi baada ya upasuaji wa kwanza.

Amesema madaktari wamemwambia ni hatari kuondoa kipandikizi hicho ambacho bado kinamletea shida.

vipandikizi hivyo vimesababisha maumivu na hali ya kudhoofika.

Image caption Bi Williams ambaye ni mwathirika wa upasuaji huo anasema Jopo la wataalam halijatoa mapendekezo ya kutosha

Siku ya ijumaa, ripoti ya jopo la wataalam kwa niaba ya serikali ya Wales ilisema njia za kuzuia tatizo zisisitizwe kutumika kuliko tiba ya kupandikiza.

Bi Williams ameitaka serikali ifanye uchunguzi kutazama idadi ya madhara ambayo wagonjwa wanayapitia baada ya upasuaji.

''Nataka ipigwe marufuku, Mimi na watu wengine wengi tunataka kuona upasuaji huu ukipigwa marufuku duniani''.

Vipandikizi,ambavyo viko vya aina tofauti vya utepe wa plastiki na vitanzi, vinatumika kupambana na matatizo ya kushindwa kuzuia haja ndogo na kusaidia viungo kama uke, mji wa mimba,kibofu cha mkojo ambavyo hushuka chini baada ya kujifungua.

Mamia ya wanawake nchini Uingereza wanachukua hatua za kisheria dhidi ya Taasisi ya huduma za afya ya umma nchini Uingereza baada ya kupata madhara.

Serikali ya Uingereza inafanya ychunguzi kubaini ni kwa kiasi gani vipandikizi hivyo vimeleta madhara.

Waziri wa Afya wa Wales Vaughan Gething atatoa taarifa Jumanne.