Maafisa wamsaka Chui aliyemla mtoto kwenye mbuga Uganda

Chui, mnyama hatari na mwenye kasi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chui ni mnyama hatari na mwenye kasi

Maafisa wa nyama pori nchini Uganda bado wanamsaka chui aliyemla mtoto wa miaka mitatu wa mwangalizi wa hifadhi ya taifa ya Malkia Elizabeth Ijumaa usiku, Shirika la habari la Ufaransa la AFP limeripoti.

Elisha Nabugyere alimfuata mlezi wake nje ya nyumba za wafanyakazi ambazo hazina uzio, ndipo chui alipomnyaka.

''Msaidizi hakujua kama mtoto alikuwa akimfuata. Alimsikia akipiga kelele akiomba msaada. Alijitahidi kumuokoa lakini alikuwa amechelewa kwani chui alishatokomea naye, msako ulianza siku ya pili tulipata fuvu la mtoto," msemaji wa mamlaja ya hifadhi nchini Uganda Bashir Hangi alieleza.

''Msako unaendelea ili kumpata chui na kumuondoa kwenye hifadhi kwa sababu kwa kuwa amekula nyama ya binaadamu, shauku ya kuendelea kula wengine itaongezeka, hivyo amekuwa mnyama hatari.Alieleza

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii