Watu 30 wafariki Kenya baada ya bwawa kuvunja kingo zake
Huwezi kusikiliza tena

Watu zaidi ya 30 wafariki Kenya baada ya bwawa kuvunja kingo zake

Mmoja ya walioshuhudia maafa ya kupasuka kwa bwawa nchini Kenya anasema kuwa wamepata miili iliofukiwa katika matope.

‘’Tulipata miili 11 iliokuwa imefukiwa na matope katika shamba moja la kahawa na hawa ni watu ambao huenda walikuwa wakitoroka lakini hawakufanikiwa kutokana na nguvu na kasi ya maji kutoka kwa bwawa hilo’’ ,alisema.

Wengi wao ni wawawake na watoto ambao hawakuweza kukimbia kwa kasi pamoja na wazee.

Mada zinazohusiana