'Hapana, ahsante sina haja', Zari Hassan amjibu msanii wa Kenya

Mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan
Image caption Mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan

'Hapana, Ahsante sina haja', ndio majibu ya Zari Hassan aliyekuwa mpenziwe nyota wa muziki wa bongo nchini Tanzania Diamond Platinumz kwa msanii wa muziki wa Injili nchini Kenya Rington baada ya mwimbaji huyo kudai kumnunulia zawadi ya gari la aina ya Range Rover Sport.

Akizungumza katika runinga ya Citizen nchini Kenya katika kipindi cha muziki cha 10 Over 10 Ijumaa usiku, Zari alisema kuwa mwimbaji huyo hajawasiliana naye.

''Nilikuja kumjua mwimbaji huyu nilipoingia nchini Kenya'' , alisema mfanyibiashara huyo wa Uganda.

Hatahivyo Zari alisema kuwa amefurahishwa na ujasiri wa Rington kujitokeza hadharani na kutaka awe mpenziwe.

Lakini alipokuwa akimpuuzilia mbali Rington , Zari alisema kuwa ana fedha za kutosha kujinunulia gari analotaka ikiwemo lile la aina ya Range Rover ambalo alinunua wiki iliopita.

Rington amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya kudai kwamba yuko tayari kumuoa mama huyo wa watoto watano, ambaye aliwachana na Diamond Platinumz siku ya wapendanao ya Valentine mwaka huu.

Inadaiwa kuwa Ringtone alitaka kumpatia gari hilo Zari lakini kwa bahati mbaya akamkosa katika eneo moja huko Westalnds

Katika kipidi hicho Zari pia alisema kuwa hayuko tayari kuanza uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote akisema kuwa anatumia muda wake kuangalia wanawe watano.

''Ninapopenda napenda kwa moyo wangu wote. Nataka kusalia bila mpenzi mwaka huu. hatahivyo iwapo nitapenda tena, mpenzi wangu hatakuwa mtu maarufu'', alisema.

Mada zinazohusiana