Watu 9 waumeuwa nchini Indonesia baada ya makanisa kushambuliwa kwa mabomu

Mashambulio hayo yalifuatana Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mashambulio hayo yalifuatana

Wahanga wa kujitoa kufa, wamevamia makanisa matatu nchini Indonsia na kuyalipua kwa mabomu.

Milipuko hiyo imetokea katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Surabaya na kusababisha vifo vya watu 9, huku idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka.

Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kutoka idara ya polisi.

Zaidi ya watu 13 wamepata majeraha, baadhi yao mabaya sana. Misururu ya milipuko hiyo ya mabomu yalifuatana.

Hakuna kundi lolote lilokiri kuhusika katika mashambulio hayo, lakini kundi linalojiita Jemaah Ansharut Daulah (JAD), ambalo lina uhusiano na kundi la wapiganaji wa kigaidi wa Islamic State, huenda lilihusika.

Picha za runinga, zinaonesha mabaki ya vitu mbalimbali yakiwa yametapakaa nje ya lango kuu la Kanisa moja lililolipuliwa.

Image caption Ramani ya taifa la Indonesia

Taarifa kwa vyombo vya habari zinasema kamba, jaribio la kulipua kanisa la nne lilitibuliwa na maafisa wa usalama.

Mashambulio hayo yanaminika kutekelezwa na Kundi la Islamic State linalojiita Jemaah Ansharut Daulah (JAD).

Katika miezi ya hivi karibuni, makundi ya waislamu wenye itikadi kali, yameongezeka sana nchini Indonesia.Katika miezi ya hivi karibuni, taifa la Indonesia, ambalo lina idadi kubwa ya waislamu, limekuwa likishuhudia misururu ya visa vya wanamgambo wenye itikadi kali ya kiislamu.