Wanafamilia watekeleza mashambulizi dhidi ya makanisa Indonesia

Indonesia, yenye waislamu wengi zaidi, imeshuhudia vitendo vya kigaidi katika miezi ya karibuni Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Indonesia, yenye waislamu wengi zaidi, imeshuhudia vitendo vya kigaidi katika miezi ya karibuni

Watu wa familia moja wanadaiwa kutekeleza mashambulizi yaliyolenga makanisa matatu nchini Indonesia

Takriban watu 13 wameuawa baada Watu waliojitoa muhanga wameshambulia makanisa matatu nchini Indonesia katika mji wa pili kwa ukubwa,Surabaya.

takriban watu 40 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo, ambayo yalitokea ndani ya dakika chache kwa kila tukio moja.

Baba wa familia aliendesha gari lililotegwa bomu kwenye viwanja vya kanisa la Pentekoste.

Mama na mabinti zake wenye umri wa miaka 9 na 12 walikuwa wamefungwa mabomu na wakajilipua kwenye kanisa la Kikistro la Diponegoro

Watoto wa kiume wa familia hiyo wenye miaka 16 na 18 waliendesha pikipiki mpaka kanisa la Mtakatifu Maria, kulipua vilipuzi walivyovibeba, shambulio lao lilikuwa la kwanza, mengine mawili yalifuata kila baada ya dakika tano.Polisi walieleza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi waliwasaidia watu waliokuwa wakiwatafuta wapendwa wao baada ya shambulio

Picha za Televisheni zimeonyesha mabaki yakiwa yamesambaa kwenye eneo la kuingilia kanisani.

Indonesia, yenye waislamu wengi zaidi, imeshuhudia vitendo vya kigaidi katika miezi ya karibuni.

zaidi ya asilimia 90 ya raia wa Indonesia ni waislamu, lakini kuna wengine walio wakristo , madhehebu ya Hindu na Budha.

Mashambulizi haya ya sasa ni makubwa zaidi tangu kutokea mwaka 2005, wakati mashambulio matatu ya kujitoa muhanga yalipotekelezwa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mashambulizi yote matatu yalifuatana

Ripoti za shuhuda ambazo hazijathibitishwa zinasema shambulio la tatu lilitekelezwa na mwanamke au wanawake kadhaa waliokuwa wamevaa ushungi na kuingia kanisani wakiwa na watoto.

Maafisa wameripotiwa kufanya jitihada za kuzuia mashambulizi mengine dhidi ya makanisa.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililokiri kufanya mashambulizi hayo.

Lakini Afisa wa shirika la intelijensia nchini Indonesia, amesema kundi la Jemaah Ansharut Daulah (JAD) linashukiwa kutekeleza mashambulizi.

Mada zinazohusiana