Marekani;Sherehe za uzinduzi wa msikiti zazua gumzo baada ya kualikwa wanaume pekee

Jabin Ahmed Ruhii anasema malalamiko yake mtandaoni yalifanya jamii ijadili Haki miliki ya picha JABIN AHMED RUHII
Image caption Jabin Ahmed Ruhii anasema malalamiko yake mtandaoni yalifanya jamii ijadili

Jamii ndogo ya waislamu mjini New York imekuwa kwenye mjadala mkali kuhusu nafasi ya wanawake, baada ya mwanamke mmoja kwenye mitandao ya kijamii kutaka mabadiliko yafanyike.

wakiwa hawana msikiti wao kwa zaidi ya miaka 20, walikuwa tayari kufanya jitihada ya kupata eneo lao wenyewe

walipopata ardhi mwaka 2007, jamii hiyo ilitumia miaka kadhaa kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi.Sasa kutokana na michango hiyo kutoka familia za wafanya kazi waliweza kulipa gharama za ujenzi kwa awamu, muda ulikuwa umewadia wa kujenga msikiti.

Jamii ilikusanyika siku ya jumapili katika sherehe za kuweka jiwe la msingi, viongozi mbali mbali walialikwa, hotuba zilitolewa na mradi wa dola milioni 1.5, jengo la orofa tatu ukawekwa wazi.

Lakini wanawake wa jamii hiyo hawakuonekana kwenye sherehe hizo wengi wao walihusika kwenye uchangiaji.

Mwanamke mmoja wa kiislamu Jabin Ahmed Ruhii alipeleka malalamiko kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Haki miliki ya picha DANIEL ZUCKERMAN/COLUMBIA-GREENE MEDIA
Image caption Sherehe za uzinduzi wa kituo cha Kiislamu

''Ingawa barua ya mwaliko ilisema ''wapendwa makaka na madada'' ,wanaume waliambiwa kuwa wanawake si sehemu ya kusanyiko hilo.alieleza . Ruhii ,24 ameeleza kuwa kitendo hicho n cha ''unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.

''Uislamu ni wa kila mmoja, si tu wanaume, Ruhii aliandika. ''Wanawake katika jamii hii wamekuwa wakikihudumia kituo hiki cha kiislamu kwa chochote wanachokuwanacho, bila kuambiwa au kukaribishwa na kaka zetu wa kiislamu.

Amesema wanawake ''wangeendelea kukiunga mkono'' kituo''bila kujali kama wanakaribishwa au la.

Rais wa kituo hicho, Abdul Hannan, amesema kuwa kutokuwepo kwa wanaume kwenye sherehe hizo jumesababishwa na ''kutokuwepo kwa mawasiliano''

Hannan anasema hakukuwa na nafasi ya kutosha kwa wanawake na kwa sababu za usalama, hivyo si wanajumuia wote wa kiislamu walioalikwa.

Hata hivyo, maafisa wengi waliofika na kuzungumza katika sherehe hiyo walikuwa wanawake

Katiba ya kituo cha kiislamu inawazuia wanawake kuwania nafasi mbalimbali hivyo hakuna uwakilishi wa wanawake kwenye bodi.

Wiki moja baada ya kuandika, yeye na wengina walialikwa na utawala wa kituo hicho kwa ajili ya majadiliano.

Wanawake 15 wapiganaji wa IS wahukumiwa kifo Iraq

''Tuliwaambia wanawake katika jamii yenu hawaoni kama wanakubalika'' Ruthii alieleza.''hamjafungua milango kwa ajili yetu.''

Hannan anaamini mkutano ulikwenda vizuri.

''Aliamini alihitaji kuongea nasi badala ya kuweka facebook, alieleza.

Kamati imeahidi kufanya tukio jingine wakati mwingine ambapo kila mtu ataalikwa.Kituo hicho pia kinafanya jitihada kuabadili katiba kuwaruhusu wanawake kuwania nafasi mbalimbali kwenye kamati.Alieleza Hannan.

Ruhii anasema mkutano ulikuwa mgumu lakini wenye heshima na kusema kuwa Hannan alifanya jitihada za kutuliza hali.Lakini anaamini kuwa kuweka malalamiko yake Facebook, kwani bila kufanya hivyo na kutikisa jamii ya kiislamu na msikiti, kusingekuwa na mazungumzo yeyote.

Mada zinazohusiana