Raia wawili wa Uingereza waliotekwa DRC waachiwa

Walinzi wanane wameuawa katika hifadhi ya taifa ya Virunga mwaka 2018 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Walinzi wanane wameuawa katika hifadhi ya taifa ya Virunga mwaka 2018

Raia wawili wa Uingereza waliokuwa wakishikiliwa mateka nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) wameachiwa huru wakiwa hawajadhurika. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson ameeleza.

Ameshukuru jitihada za serikali ya DRC na Taasisi ya hifadhi za asili kwa msaada wao wa kuwatafuta bila kuchoka.

Raia hao kwa sasa wanapatiwa huduma za kitabibu, kwa mujibu wa taarifa ya hifadhi ya taifa ya Virunga.

Mwangalizi wa hifadhi hiyo aliyeuawa na watekaji nyara ametambulika kwa jina la Rachel Masika Baraka.

Watalii wa Uingereza watekwa nyara DR Congo

Dereva wao alijeruhiwa na aliachiwa muda mfupi baada ya utekaji, uliofanyika katika kijiji cha Kibati, Kaskazini mwa mji wa Goma, asubuhi ya tarehe 11 mwezi Mei.

Mwezi April BBC Ilielezwa kuwa mashambulizi yanayojitokeza ni sehemu ya uhalifu unaohusisha uporaji na usafirishaji wa maliasili.

Maafisa walisema hifadhi inalindwa na waangalizi 800 lakini inaelezwa kuwa kuna wanamgambo 1,500 na 2000 ndani na kuzunguka hifadhi.

mamlaka ya hifadhi imesema mwezi uliopita waangalizi watano na dereva waliuawa na wanamgambo.

lilikuwa tukio baya sana kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni,Idadi ya walinzi wa eneo hilo waliouawa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita ni 175.

Mada zinazohusiana