Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 14.05.2018

Wilfried Zaha Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wilfried Zaha

Wing'a raia wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 25, anasena hana nia ya ya kuhama Crystal Palace msimu huu. (Express)

Everton na West Ham wote wanamwinda meneja wa zamani wa Hull na Watford Marco Silva. (Mirror)

Wamiliki wa Swansea wamemuuliza Carlos Carvalhal iwapo yuko tayari kuwaongoza. (Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema anamtakia mema kocha Mikel Arteta huku kukiendelra na uvumi kuwa Arteta 36, anatarajiwa kuchukua mahala pake Arsene Wenger. (Metro)

Kipa wa Slovakia Martin Dubravka, 29, atafanya mazungumzo na Newcastle United siku zinazokuja baada ya kumaliza mkopo wake kutoka Sparta Prague.(Chronicle Live)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Claude Puel

Meneja wa Leicester Claude Puel amesema kuwa ataheshimu mkataba wake na klabu hiyo licha ya uvumi kuwa anatafutwa na klabu ya Ufaransa Saint-Etienne. (Leicester Mercury)

Meneja wa Everton Sam Allardyce amesema hakuna mzozo kati yake na Wayne Rooney, wakati mchezaji huyo wa miaka 32 anahusihswa na klabu ya ligi kuu ya soka ya DC United. (Talksport)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption David Wagner

David Wagner amekataa kutoa hakikisho lolote kuhusu hatma yake kama meneja wa Huddersfield licha ya mwenyekiti wake Dean Hoyle kusema atasalia katika klabu hiyo. (Mirror)

Mashabiki wa AC Milan walikataa kuchukua shati lake kipa wa miaka 19 raia wa Italia Gianluigi Donnarumma wakati wa kumalizika kwa mechi ya siku ya Jumamosi na Atalanta. (Calciomercato via La Gazzetta dello Sport)

Mchezaji wa zamani wa Stoke Dominic Matteo anaamini klabu hiyo ingemfuta meneja Mark Hughes mapema ili kuzuia klabu hiyo kuzushwa kutoka kwa Premier League. (Inside Futbol)

Bora kutoka Jumapili

Manchester United wana mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar huku klabu hiyo ya Old Trafford ikipambana na Real Madrid kupata sahihi ya mchezaji huyo 26 mwenye asili ya Brazil (Sunday Mirror)

Unai Emery, ambaye ataondoka Paris St-Germain mwishoni mwa msimu, amekuwa gumzo, akipendekezwa kuchukua mikoba ya Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal (Sunday Express)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Masimilliano Allegri akiwa amembeba Juan Cuadrado

Hata hivyo, West Ham wanamhitaji Emery achukue mikoba ya David Moyes. Meneja wa zamani wa Manchester City Manuel Pellegrini na meneja wa zamani wa Watford Marco Silva wanamtamani Emery.(Sun on Sunday)

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri, anataka kitita cha pauni milioni 200 kama atakuwa meneja wa Arsenal.(Sun on Sunday)

Manchester City inataka saini ya kiungo wa kati wa Napoli,Jorginho, 26, na mshambuliaji wa pembeni Riyad Mahrez, 27, wa Leicester kwa gharama ya takriban pauni milioni 110 (Mail on Sunday)