Maandamano zaidi kushuhudiwa Gaza leo Jumanne

Emergency services and Palestinians carry a wounded protestor during clashes with Israeli security forces near the border between Israel and the Gaza Strip, east of Jabalia on May 14, 2018 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Takriban watu 2,700 walijeruhiwa kwa mujibu wa maafisa wa Palestina

Maandamano mapya dhidi ya Israel yanatarajiwa huko Palestina leo Jumanne, siku moja baada ya wanajeshi kuwaua watu 58 huko ukanda wa Gaza.

Jumatatu ilikuwa siku mbaya zaidi tangu maandamano kuanza kwenye mpaka wa Gaza wiki saba zilizopita.

Leo itakuwa ni maadhimisho ya miaka 70 ambayo Wapalestina wanayataja kama Nakba - ambayo ni maadhimisho ya kuhamishwa kwa Wapalestina kufuatia vita vya kuundwa kwa Israel.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ivanka Trump kwenye sherehe ya kufunguliwa ubalozi wa Marekani

Msukosuko mpya unatarajiwa huko Gaza siku ambayo yatafanyika maziko ya wale waliouawa.

Ghasia za Jumatatu zilizuka wakati ambapo Marekani ilikuwa inafungua ubalozi wake huko Jerusalem hatua iligadhabisha wapalestina.

Wanadai Jerusalem Mashariki ni mji mkuu wa taifa la baadaye la Palestina na kuitaja hatua ya Maeekani kama inayounga mkono Israel kuweza kudhibiti mji huo wote inaoutaja kuwa mji wake mkuu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji wa Palestina

Maafisa wa Palestina wanasema takriban watu 2,700 walijeruhiwa wakati wa ghasia hizo siku ya Jumataua - zilizo mbaya zaidi kuwai kushuhudiwa huko Gaza tangu mwaka 2014.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema jeshi lake lilikuwa linajilinda dhidi ya watawala wa Gaza, Hamas ambao anasema lengo lako ni kuiangamiza Israel.

Israeli PM Benjamin Netanyahu said his military was acting in self-defence against Gaza's Islamist rulers, Hamas, who he said wanted to destroy Israel.

Kipi kilitokea mpakani?

Wapalestina walikuwa wanaandamana siku ya Jumatatua jinsi wamekuwa wakiandana kwa wiki sita katika sehemu ya maandamano yaliyochochewa na Hamas yanaofahamika kama "Great March of Return".

Hata hivyo yale ya Jumatatua na leo Jumanne yanakwenda sambamba na maadhimisho ya kuundwa taifa la Isreal mwaka 1948 na kuhama maelfu ya wapalestina kutokana na vita vilivyofuatia.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Takribana watu 2,700 walijeruhiwa

Mada zinazohusiana