Wanawake Kenya waandamana kwa hasira kushinikiza haki ya mama kumyonyesha mwana Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake Kenya waandamana kwa hasira kushinikiza haki ya mama kumyonyesha mwana

Wanawake wameandamana leo Nairobi kulalamika kufukuzwa kwa mama aliyemnyonyesha mwanawe katika mgahawa mmoja mjini. Taarifa hiyo imezusha hisia kali kote nchini na kusababisha makundi ya kutetea haki za wanawake kuandaa maandamano ya leo mjini. Dhamira kuu ni kushinikiza haki za akina mama waungwe mkono na kusaidiwa katika kufanikisha kuwanyonyesha watoto wao bila ya ubaguzi wa aina yoyote.