Rais wa nchi ya watu wawili afariki dunia akitibiwa Israel

Eli Avivi, the head of self proclaimed micro-nation, pictured in 2006 Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Rais Eli Avivi, akiwa Achzivland mwaka 2006

Mmoja wa watawala wa miaka mingi zaidi huko Mashariki ya Kati amefariki dunia akiwa na miaka 88 lakini Eli Avivi hakuwa rais wa kawaida tu.

Aliongoza taifa hilo zaidi la Achzivlabd lenye watu wawili kwa karibu nusu karne.

Taifa hilo dogo lililo kaskazini mwa Israel karibu na mpaka na Lebanon, liliwavutia watu mashuhuri wakiwemo Sophia Loren.

Licha ya kutotambuliwa kimataifa, lina bendera yake na wimbo wa taifa.

Aviv ameacha mjane ambaye pia ndiye raia pekee wa Achzivland Rina, 71, ambaye alithibitisha kifo chake mapema Jumatano.

Dada yale aliambia mtandao mmoja wa habari nchini Isreal kwa amekuwa akiugua kichomi.

Eli Avivi alikuwa ni nani?

Alizaliwa huko Persia na kuhamia eneo lililokuwa linatawaliwa na Uingereza la kipalesina akiwa na umri wa miaka mwili.

Alijunga na jeshi na wanamaji la kiyahudi lililofahamika kama the Palyan akiwa na miaka 15 na kupigana dhidi ya jeshi la Uingereza na baadaye dhidi ya vikosi vya kiarabu wakati wa vita vya mwaka 1948.

Eneo lililokuja kuwa Achzivland kilikuwa ni kijiji cha uvuvi cha kipalestina kinachofahamika kama al-Zeeb ambacho wakaazi wake walikimbia wakati kilishindwa mwaka 1948.

Avivi aligundua eneo hilo miaka minne baadaye na kuishi kwenye majengo yaliyokuwa yameharibiwa akiendelea na maisha akiuza samaki. Baadaye Rina aliwasili na na Avivi akamuoa.

Wawili hao waliendelea kuwa na matatizo na Israel kuanzia miaka ya sitini wakati serikali iliamua kubadili eneo hilo kuwa mbuga ya taifa na kutuma tinga tinga kubomaa majengo.

Hali iligeuka kuwa mbaya wakati mamlaka ziliweka ua kulizingira eneo hilo na kumzuua Avivi kulifikia. Akipinga hilo Eli na mke wake walichana pasipoti zao na kutangaza uhuru kutoka Israel mwaka 1971.

Kukamatwa kwao na kesi dhidi yao vilisababisha wapate umaarufu mkubwa pamoja na eneo la Achzivland.

Wawili hao baadaye wakaafikia makubaliano na Israel kulipa kuweza kuingia eneo hilo. Wajitengenezea pasipoti zoa na wangeweza kupiga muhubi zile za wageni ambao wangezuru eneo hilo la ekari 3.5.

Miaka iliyofuatia, wageni kutoka kote duniani walizuru moja ya nchi ndogo zaidi duniani isiyotambuliwa.

Hatma ya Achzivland ni ipi?

Haijulikani kile kitafuatia bila ya kuwepo raia wake.

Wakati wa mahojiano na BBC mwaka 2015 Avivi alisema hakufikiri alikuwa na miaka zaidi ya kuishi. Alisema alitumai Rina atabaki eneo hilo lakini pia ulikuwa ni uamuzi wake.

Anataka eneo hilo kuwa makumbusho kwa mumewe anayemtaja kuwa rais bora zaidi kuwai kuwepo.

Image caption Ramani ya Achzivland

Mada zinazohusiana