Treni iliyokuwa ikisafirisha mafuta yapata ajali Mombasa

Wanajeshi nchini Kenya wamelazimika kutoa msaada wa uokozi baada ya Treni iliyokuwa ikisafirisha mafuta yapata ajali katika eneo la Kibarani jana jumapili.

Ajali hiyo ilisababisha kukata kwa wasiliano ya barabara kati ya mji wa Mombasa na Nairobi na kuathiri mamia ya mabasi ya Abiria.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Mombasa Bw. Johnston Ipara amesema waliwatumia wanajeshi hao ili kudhibiti hali na kukinga majeruhi kutokea katika eneo hilo.

Johnston amewasihi watu wote wanaoishi katika eneo hilo kutowasha moto na wamewahamisha watu walikuwa wakiishi karibu na sehemu hiyo.