Nemanja Matic: Man Utd inaweza 'kulipigania taji la ligi na ubingwa wa Ulaya' iwapo itasajili wachezaji wastahiki.

Nemanja Matic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nemanja Matic played 48 times for Manchester United this season

Manchester United inaweza 'kulipigania taji la ligi na ubingwa wa Ulaya' iwapo itasajili wachezaji wastahiki msimu huu wa joto, anasema mchezaji wa kiungo cha kati Nemanja Matic.

United ilinyukwa katika fainali za kombe la FA mwishoni mwa juma dhidi ya Chelsea kwa 1-0 na kuishia katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya England, pointi 19 nyuma ya Manchester City.

Hiyo ni baada ya klabu hiyo kutumia gharama ya £148m katika uhamisho msimu uliopita wa joto, ikiwemo usajili wenye gharama kubwa wa Matic na Romelu Lukaku.

Matic amesema wachezaji walio na "uzoefu" wanahitajika kuleta "ubora zaidi".

"Timu iliyo bora kuliko yetu mwaka huu ni Manchester City," amesema mchezaji huyo raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 29.

Maelezo ya video,

Jose Mourinho alalama hakuna anayeishabikia Man United

"Ni wazi kwamba wanacheza soka nzuri. Lakini sisi ni wa pili na tuko katika ligi ya mabingwa mwaka ujao, ambalo ndilo jambo muhimu."

United imetumia £261.67m katika misimu miwili iliyopita - £98.37m chini ya City - ikishikilia kwa wakati huo rekodi ya dunia ya gharama kubwa aliyolipiwa mchezaji - Paul Pogba mnamo 2016.

Mshambuliaji Lukaku alijiunga kwa gharama ya milioni £75 msimu uliopita wa joto na Matic alielekea Old Trafford kwa milioni £40.

Kulikuwana makubaliano mengine yenye gharama kubwa ikiwemo uhamisho wa Victor Lindelof ana mchezaji mwenzake wa kati beki Eric Bailly, huku mchezaji wa kiungo cha mbele Alexis Sanchez alihama kutoka Arsenal mnamo Januari.

"Tunahitaji baadhi ya wachezaji walio na uzoefu ili kuleta ubora zaidi katika timu yetu," aliongeza mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea Matic.

"Baada ya hapo, tunaweza kulipagnia taji na ligi ya ubongwa pia. Nadhani tumeimarika."

United ilishinda taji mwisho mnamo 2013 katika msimu wa mwisho wa Sir Alex Ferguson' na tangu hapo wameibuka nambari saba, nne, tano na sita kabla ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu huu.