Marekani: Tutaiwekea Iran vikwazo vya kihistoria

Rais Rouhan apinga vikwazo vya Marekani

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Rais Rouhan apinga vikwazo vya Marekani

Rais wa Iran Hassan Rouhani, amepinga vikali kauli ya Marekani iliyotolewa na waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo, aliyesema kuwa taifa lake linatarajia kuiwekea Irani vikwazo ambavyo havijawahi kuvipitia katika historia ya taifa hilo.

Rouhani amesema Pompeo, alipokuwa mkuu wa shirika la upelelezi la CIA, alishawahi shinikiza kuwekwa vikwazo dhidi ya taifa hilo ili kuachana na silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu.

Wewe ni nani? uweze kuwa na maamuzi dhidi ya Iran na dunia? amefoka Rais Rouhan, akiongeza kuwa Pompeo kwa mara nyingine shinikizo alilowahi lisimamia dhidi ya taifa hilo akiwa mkuu wa shirika la upepelezi la CIA wakati huo.

Amesema kuwa Iran kamwe tena namna yoyote mkono wa mtu kuishikilia mashariki ya kati.Kwa upande wake waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu,amepongeza kauli ya bwana Pompeo na uungwaji mkono wa Marekani kimataifa.

"Tunaamini hii ndiyo sera nzuri.Ni sera pekee inayoweza kutuhakikishia usalama wa mashariki ya kati katika ukanda wetu.Na tunatoa wito kwa mataifa yote kufuata msimamo wa Marekani kwa sababu Irani ina nguvu za uchokozi."Netanyahu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Iran ilipunguza shughuli zake za nyuklia ili iondolewe vikwazo

Pompeo ametaja mambo kumi na mbili ambayo Washington inautaka utawala wa Tehran kufanya,ikiwa ni pamoja na suala la Iran kuondoa vikosi vyake, Syria na kusitisha misaada kwa waasi wa Yemen. Amesisitiza kwa mataifa yanapaswa kuunga mkono hatua hizo za Marekani.

Kwa mikakati iliyowekwa hii leo,tunahitaji uungwaji mkono na washirika wetu ndani ya ukanda wetu na marafiki zetu wa Ulaya pia kutuunga mkono kukabiliana na Iran.

Ametishia pia kwamba mataifa yatakayokiuka masharti ya vikwazo dhidi ya Iran,kwamba yatakumbana na hali ngumu.

''Tunaelewa kuwa hatua yetu ya kuweka tena vikwazo dhidi ya utawala la Iran itasababisha ugumu wa kiuchumi kwa baadhi ya rafiki zetu,tunahitaji kusikia hoja zao,lakini mjue kuwa tutazuia biashara zilizokatazwa kufanyika na Iran.kwa wiki chache zijazo tuta tuma timu ya watalaam duniani kwaajili ya ufafanuzi sera za utawala,ma na matokeo na kujadili matokeo ya vikwazo hivi,Najua nimetumia muda mwingi ndani ya wiki tatu kukaa na washirika wetu na kujadili kwa kina.Najua wanaweza kujaribu kuendeleza mahusiano ya masuala ya nyuklia na Iran,huo ni uamuzi wao,lakini wanajua msimamo wetu''.Pompeo