Zimbabwe yaomba kujiunga tena na Jumuiya ya Madola

Mnangawa anasema anataka kujenga ushirikiano wa kimataifa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mnangawa anasema anataka kujenga ushirikiano wa kimataifa

Zimbabwe imetuma maombi ya kujiunga tena kwenye Jumuiya ya Madola miaka 15 tangu iondoke Jumuiya hiyo.

Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Patricia Scotland, alisema alifurahishwa kupata barua kutoka kwa Rais wa Zimabawe Emmerson Mnangagwa iliyoandikwa tarehe 15 mwezi Mei.

Hata hivyo alisema kuwa Zimbabwe itarudi wakati masharti yatatimizwa.

Rais Mnangagwa ambaye aliingia madarakani mwezi Novemba baada ya kuondolewa kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, amesema mara kwa mara kuwa anataka kujenga uhusiano wa kimataifa.

Ni nini Jumuiya ya madola?

  • Ni muungano wa mataifa yaliokuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Uingereza, na mataifa mengine pia.
  • Ilianzishwa mnamo 1931
  • Kuna mataifa wanachama 53
  • Makao yake makuu yapo London
  • Takriban watu bilioni 2.4 wanaishi katika mataifa ya jumuiya ya madola

Zimbabwe ilijitoa kwa Jumuiya hiyo ya nchi 53 mwaka 2003 baada ya kujiunga nayo mwaka 1980.

Mugabe alikataa jitihada za awali za kuirejesha Zimbabwe katika Jumuiya hiyo.

Maelezo ya picha,

Rais wa zamani Robert Mugabe alikataa jitihada za awali za kuirejesha Zimbabwe katika Jumuiya hiyo.

Taarifa ya Jumiya ya Madola inasema kuwa nchi hiyo itahitaji kutumaiia maala yamsuala kadhaa yakimwei demoksraia na shmna na opamija na kulinna haki za bidamu, h=uhuru wa kujieleza kabala ya kuruhsuwia kujunga tena.

Waangalizi kutoka Jumuiya hiyo wamealikwa kwenye uchaguzi wa Zimbabwe katika kile kitanaonekana kama sehemu ya mchakato wa kuirejesha Zimbawe kwenye Jumuiya ya Madola.

Nchi zilizorudi upya katika Jumuiya ya madola

Baada ya Afrika kusini, Pakistan na Fiji, sasa Gambia inakuwa nchi ya nne kurudi katika jumuiya ya madola.

Afrika kusini ilitangaza kujitoa katika jumuiya hiyo mnamo Mei mwaka 1961 baada ya kupitisha sheria ilioifanya nchi hiyo kuwa Jamhuri na kusitisha utawala wa malkia.

Ilijunga upya miaka 33 baadaye mnamo 1994 baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini.

Mnamo 2008 Jumuiya ya madola ilikubali kuirudisha Pakistan mwaka mmoja baada ya kuusitishauwanachama wake kufuatia hatua ya kiongozi aliyekuwepo Pervez Musharaf kuidhinisha hali ya hatari na kuwazuia maelfu ya wanaharakati wa upinzani.

Gambia ilijiunga na jumuiya ya madola kwa mara ya kwanza mnamo 1965, muda mfupi tu baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza.

Ombi la Gabon mwaka jana kurudi katika jumuiya ya madola liliitikiwa na wengi, na sasa Gambia imerudi rasmi na imealikwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa serikali wa jumuiya ya madola huko London mwezi Aprili.