Ripoti:Vitendo vya uharamia viliongezeka mwaka 2017

Uharamia umekuwa tishio kwa safari za majini katika ukanda wa pwani wa Afrika

Chanzo cha picha, One earth report

Maelezo ya picha,

Uharamia umekuwa tishio kwa safari za majini katika ukanda wa pwani wa Afrika

Idadi ya vitendo vya uharamia pwani ya Afrika mashariki iliongezeka mara mbili mwaka 2017 ukilinganisha na mwaka 2016, Vyombo vya kimataifa vinavyoshughulikia usalama wa majini vimeeleza.

Ilioyesha kuwa mtandao wa uhalifu nchini Somalia ulikuwa bado una uwezo wa utekeleza mashambulizi.

Vitendo vya uharamia mwaka 2017 vinaonyesha wazi kuwa makundi haya yameendelea kuwa na uwezo wa kuratibu na kutekeleza mashambulizi dhidi ya Meli zinazosafiri kwenye eneo la Afrika .

Phil Belcher kutoka kwenye taasisi ya Intertanko amesema mgogoro nchini Yemen pia ulikuwa ukitishia usafirishaji wa majini karibu na eneo la pembe ya Afrika

''Tunawashauri washirika wetu kuja na mbinu madhubuti za kiusalama ili kudhibiti vitisho vingine.

Uharamia umeendelea kuwa tishio katika rasi ya Guinea ingawa hatua mbalimbali zimechukuliwa katika maeneo ya pwani na makampuni ya ulinzi wa majini, imeeleza ripoti hiyo

Meli ya Korea Kusini Munmu ili tumwa tena katika eneo la rasi ya Guinea baada ya wavuvi watatu wa Korea Kusini kutekwa mwezi Machi.Utekaji nyara kwa ajili ya kujipatia pesa umeendeleza kukumba eneo hili, ambapo imezoeleka kuwa hivyo kwa bahari mbaya kuanzia mwaka 2016, alieleza Maisie Pigeon,mwandishi wa ripoti hiyo.

Ripoti imebaini kuwa wafanyakazi 100 walitekwa nyara mwaka 2016.

Chanzo cha picha, EUROPEAN UNION NAVAL FORCE

Maelezo ya picha,

Uharamia wenye lengo la kujipatia pesa uepungua

Uharamia katika pwani ya Somalia ambao mara nyingi hufanyika kwa ajili ya kujipatia pesa umepungua kwa miaka ya hivi karibuni, kwa sababu ya kuwepo kwa doria za kijeshi za kimataifa pia usaidizi kwa jamii za wavuvi.

Mwaka 2011 kulikuwa na mashambulizi 237 na gharama ya fedha inakadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 8.