Mlipuko wa Ebola DRC umebadilisha maisha Kigoma?

Mataifa jirani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamekuwa katika hali ya tahadhari kubwa kuhakikisha wanadhibiti kuingia kwa virusi hivyo katika maeneo yao.

Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania unapakana na DRC na kumekuwa na mwingiliano wa watu kibiashara na kijamii.

Mwenzetu Omar Mkambara amezungumza na mwandishi wa habari Deogratius Nsokolo anayefanya kazi mkoani Kigoma, Kusini Magharibi mwa Tanzania na kwanza amemuuliza hali ikoje tangu mlipuko wa ugonjwa huo uanze.