Sababu ya visa vya uharamia kuanza kuongezeka Somalia

Visa vya uharamia katika pwani ya Somalia viliongezeka mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2016. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la The Oceans Beyond Piracy.

Ripoti hiyo inasema zaidi ya mabaharia elfu moja waliathirika katika zaidi ya visa hamsini vilivyoripotiwa.

Kufahamu zaidi hali ya usalama wa mabaharia katika ukanda wa Afrika Mashariki, hususan nchini Somalia, nimezungunmza na Andrew Mwangura ambaye ni mshirikishi wa mabaharia Afrika Mashariki.