Facebook yakiri kutowajibika vya kutosha kudhibiti udukuzi

Mark Zuckerberg aomba radhi tena udukuzi
Maelezo ya picha,

Mark Zuckerberg aomba radhi tena udukuzi

Mkuu wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg,kwa mara nyingine ameomba radhi akidai kuwa kampuni yake haijawajibika kwa kiasi cha kutosha kudhibiti baadhi ya mambo kama vile habari za uzushi katika mtandao huo,kuingilia chaguzi na taarifa binafsi za wateja wake kudukuliwa. Hii mara nyingine kwa Zuckerberg kuibuka na kuwasilisha utetezi wake.

Marck Zuckerberg akizungumza mbele ya bunge la Ulaya,ameelezea hatua ambazo Facebook imekuwa ikizichukua kuwa ni kuweka uhalali wa baadhi ya vitu ndani ya mtandao huo na kuhakikisha kuna mfumo unaolinda kudukuliwa kwa taarifa bionafsi za wateja.

''Kwa kabisa,kwa sasa unapotumia mtandao wetu,utaongozwa kwa na taarifa zako ili uweze kuingia na kupitia ukurasa wako na taarifa zake.

Jambo la pili ni kwamba kama utakuwa hujatumia mtandao wetu kwa muda wa miezi utatakiwa kuingia upya na kuonyuesha hatua za siri za usajili wako.Na tatu ni kwamba mwezi uliopita,tulionyesha program maalumu inayoonyesha wazi program nyingine na namna ya kuziruhusu ama kuzikatalia,jambo ambalo ni ulinzi kudukuliwa pia.

Maelezo ya picha,

Zuckerbag akutana na rais wa bunge la Ulaya Antonio Tajani kabla ya kuhojiwa

Na mwisho kabisa ni kwamba tunachunguza kila program ambayo tunaona kwa kiasi kikubwa inakiwango kikubwa cha taarifa binafsi za wateja wetu tangu 2014.Na pale tutakapoona kuna hali yoyote ya kutatanisha,tutawasiliana nao ama kuondoa kabisa program inayoingiliana na taarifa binafsi za wateja wetu na kuweka wazi kwa kila aliyeathirika kwamba program fulani inahusika''.Zuckerberg

Mjumbe kutoka Ubeligiji Guy Verhofstadt, amesema Zuckerberg anapaswa kufikiria na kulinda zaidi heshima yake.

''Lazima ujiulize mwenyewe kwamba unataka kukumbukwa kwa lipi,kama mmoja wa watu watatu muhimu katika masuala ya kimitandao,ambao ni Steve Jobs mwanzilishi wa appo na Bill Gates,mwanzilishi wa programu ya Microsoft na ambaye ameleta mabadiliko makubwa duniani na katika jamii yetu.Hilo ndilo jambo unalopaswa kujiuliza mwenyewe''. Guy Verhofstadt

Miaka ya hivi karibuni ilijitokeza kwamba taarifa za mamilion ya watumiaji wa Facebook,zilidukuliwa na watalaam wa kimitandao wa kambi ya kampeni ya Trump,ambapo kufuatia hali hiyo kwa mara nyingine Zuckerberg kwa mara nyingine ameomba msamaha kwa kutochukua hatua stahiki na za kutosha kudhibiti.

''Ni wazi kwamba katika miaka kadhaa iliyopita,hatukuweza kujilinda vilivyo hali iliyosababisha kudukuliwa.Na hilo ni pamoja na suala la taarifa zisizo za kweli,suala la kuingilia uchaguzi na matumizi mabaya ya taarifa za watu,hilo lilikuwa ni kosa kwetu na ninaomba radhi''.Zuckerberg

Mtandao wa Facebook kwa mjibu wa takwimu za miezi mitatu ya mwaka 2018 una watumiaji wapatao billion 2.19 ambalo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na watumiaji Bilion moja miezi mitatu ya mwanzo yam waka 2012.