Matope ya volkano yatishia kituo cha umeme Hawaii

Aerial view of lava fissure near power plant Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Matope ya volkano karibu na kituo cha umeme cha Puna

Matope kutoka mlima Kilauea huko Hawaii yameelekea kitua cha umeme, hali ambayo imewalazimisha wafanyakazi kuzima mitambo kwa hofu ya kuvuja gesi za sumu.

Wafanyakazi waliondoa bidhaa zinazoweza kushika moto kwa haraka na visima vya vyenye kina kirefu vya kituo hicho vimejazwa maji baridi na kufungwa

Ikiwa matope hayo ya volkano yataingia kwenye visima hivyo inaweza kuvuja gesi yenye sumu ya hydrogen sulphate

Matope yanayosonga kwa mwendo wa chini yaliingia eneo la kituo hicho Jumatatu na tangu wakati huo yamesimama.

Haki miliki ya picha USGS
Image caption Matope ya moto yakirushwa kutoka kwa mlima

"Hauwezi kutabiri ni wapi yataelekea au ni lini yatafika huko," afisa wa huduma za dharura za Hawaii alisema,.

Maafisa wa kaunti walisema matope hayo yako umbali wa takriban mita 270 kutoka kisima kilicho karibu.

Bw Travis alisema mvuke unaweza kutoka, kemikali kadhaa na pia gesi ya hydrogen sulphide ambayo ni hatari sana.

Watoa huduma za dharura walihamisha ndoo 60,000 na gesi yenye kushika moto kutoka kituo hicho.

Haki miliki ya picha USGS
Image caption Matoke yakisonga kusini mwa mlima Kilauea
Haki miliki ya picha USGS
Image caption Matope ya moto

Kituo hicho cha umeme huzalisha karibu asilimia 30 ya umeme unaohitajika kwenye kisiwa hicho kwa kutumia mvuke unaotoka chini ya ardhi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moshi kutoka kwa volkano

Mlima Kilauea ulilipuka mwanzo wa mwezi Mei na hali kwa wenyeji wa eneo hilo inazidi kuwa mbaya.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Matope ya volkania yaliharibu nyumba

Mada zinazohusiana