Wazazi wamshtaki mtoto wao wa kiume ambaye amekataa kuhama nyumbani

Photo of house
Maelezo ya picha,

Licha ya kumuandia barua mara tano kumtaka ahame nyumba yao Christina na Mark Rotondo wanasema mtoto huyo wao amekataa kuhama.

Wazazi wa mwanamume mmoja wa umri wa miaka 30 wametumia mbinu zisizo za kawaida kumlazimisha mto wao huyo kuhama nyumba yao.

Nyaraka za mahakama zinasema kuwa Michael Ratondo halipi kodi ya nyumba wala hasaidii na kazi za nyumbani na amepuuza msaada wa kifedha wa wazazi kutaka kumwezesha apate nyumba yake ya kuishi.

Licha ya kumuandia barua mara tano kumtaka ahame nyumba yao Christina na Mark Rotondo wanasema mtoto huyo wao amekataa kuhama.

Michael anasema kisheria hakupewa muda wa kutosha kumwezesha kuondoka.

Bi na Bw Ratondo walipeleka kesi kwenye mahakama ya Onondaga karibu na Syracue, New York tarehe saba mwezi Mei baada ya miezi kadhaa ya jitihada za kumshawishi mtoto huyo kuhama kufeli.

"Tumeamua kuwa ni lazima uondoke nyumba hii mara moja," barua moja iliyokuwa imeandikwa Februari tarehe 2 ilisema.

Wakati Michael alipuuza barua hiyo, wazazi wake waliandika tena barua ya kumuagiza ahame kwa msaada wa wakili wao.

Wanandoa hao kisha wakampa mtoto wao dola 1,100 kuondoka nyumbani pamoja na barua iliyokuwa na maneno makali kuhusu tabia yake.

"Kuna ajira nyingi hata kwa wale walio na historia mbaya ya kazi kama wewe," Tafuta moja - ni lazima ufanye kazi!" walisema.

Tarehe 30 mwezi Machi hata hivyo, imekuwa wazi kuwa mtoto huyo hana mpango wowote kuondoka

Mwezi Aprili Bw na Bi Rotondo walienda mahakamani kuona kuwa itawasaidia kumhasisha mtoto huyo wao.

Lakini waliambiwa kuwa kwa sababu Michael ni mmoja wa watu wa familia watahitaji uamuzi wa mahakama ya juu zaidi kuweza kumhamisha

Sasa familia hiyo ya Rotondo itapeleka kesi yao kwenye mahakama ya juu baadaye wiki hii siku chache kabla ya yeye kufikisha umri wa miaka 31.