Ndege yapasuka vipande viwili baada ya kuanguka Honduras

Watu wote waliokuwemo walisurika wakati ndege hiyo iliyokuwa safarini kutoka Texas ilianguka Honduras.

Maelezo ya picha,

Takriban watu sita raia wa Marekani walijeruhiwa wakati ndege iliandika kwenye mji mkuu wa Honduras

Maelezo ya picha,

Ndege hiyo ya Gulfstream G200 ilikuwa safarini kutoka Austin, Texas, wakati ilikosa barabara ya uwanja wa kimataifa wa Toncontin

Maelezo ya picha,

Mamlaka zinasema kuna ripoti za kukinzana kuhusu ni watu wanagapi walikuwa kwenye ndege hiyo

Maelezo ya picha,

Mtu mmoja aliliambia shirika la AFP kuwa aliwasaidia wanaume watano na mwanamke mmoja kuondoka kwenye ndege hiyo wakiwa na majeraha madogo

Maelezo ya picha,

Ndege hiyo ya kubinafsi ilikuwa imetumbukia kwenye bonde

Maelezo ya picha,

Ukiwa umezungukwa na milima na barabara yake ikiwa ni fupi uwanja wa Toncontin unatajwa kuwa hatari zaidi duniani

Maelezo ya picha,

Mwaka 2018 ndege ya shirika la TACA ilianguka eneo hilo hilo ambapo watu watano waliuawa

Maelezo ya picha,

Serikali inajenga uwanja mpya wa kimataifa karibu umbali wa kilomita 50 kutoka mji mkuu