Vijiji vitano Uganda viko kwenye taharuki baada ya kupata vitisho

Polisi nchini Uganda imesema imejipanga kudhibiti uhalifu dhidi ya wakazi
Maelezo ya picha,

Polisi nchini Uganda imesema imejipanga kudhibiti uhalifu dhidi ya wakazi

Hofu imetanda mjini Jinja baada ya vipeperushi vilivyo na ujumbe wa vitisho kuwa vitawashambulia wakazi vilidondoshwa na magenge ya watu wasiojulikana kwenye vijiji vitano.

Gazeti la The Daily Monitor la Uganda limeripoti kuwa vipeperushi vimedaiwa kutupwa kwenye vijiji vya Wakitaka, Kaitabawala, Namulesa, Lwanda and Sakabusolo vilivyoko umbali wa kilometa 11 kutoka mji wa Jinja.

Mwenyekiti wa Kaunti ya Mafubira, Hamis Kiganyira amesema watu hao wamewataka wakazi kuwapa pesa, huku barua nyingine zikiwataka mabinti 120 kutoa vijiji vya Namulesa na Wakitaka , matiti 20 ya watu wazima kutoka kijiji cha Lwansa na wake 400 kutoka kijiji cha Kaitabawala.

Kiganyira amesema vipeperushi, vilivyosambazwa katika eneo hilo tangu siku ya Jumapili, vinamlenga yeye pia, na kuwa vitendo ambavyo vimeleta hofu miongoni mwa wakazi licha ya Polisi kuingilia kati.

Polisi wamesema washukiwa wawili wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi dhidi ya mkazi mmoja wa kijiji cha Wakitaka.Mmoja kati ya hao alitambulika kwa jina la Majid alikamatwa akiwa na panga.Washukiwa wanashikiliwa katika kituo cha polisi mjini Jinja.

Hatua zimechukuliwa hivi sasa.Bwana Kiganyira amesema Kamati ya watu 30 ieundwa ili kutoa nguvu kwa operesheni ya usalama kwenye vijiji, huku wakazi wa vijiji wakiagizwa kuwa wamfikishe mikononi kmwa Polisi yeyote watakayemkamata akirandaranda mtaani wakati wa usiku.

Maelezo ya picha,

Watu wasiojulikana wameleta hofu kwa wakazi wa vijiji hivyo nchini Uganda

Suleiman Musoga, mkazi wa Mafubira ana hofu kuwa usalama wa familia yake, ameitaka Serikali kuweka marufuku ya kutotoka nje kwenye eneo hilo.

Mkazi mwingine ambaye amekataa kutajwa jina amesema anahofu kuwa hawako salama kwa kuwa ameona vyombo vingi vya moto hasa kipindi ambacho kulikuwa na vitendo vingi vya utekaji nyara.

Vitendo vya usambazaji wa vipeperushi vyenye vitisho mjini Jinja viafanana na vile vilivyowahi kutokea katika eneo la Masaka.

Vipeperushi vilitupwa vikiwatahadharisha wakazi wa manispaa ya Masaka kuwaandalia fedha vinginevyo watakuwa hatarini kuuawa, vikiwashinikiza wakazi kuacha makazi yao.