Amnesty International lainyooshea kidole jeshi la Nigeria

Wanajeshi wa Nigeria
Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Nigeria

Ripoti mpya ya shirika la Amnesty International iliyotolewa inalituhumu jeshi la Nigeria kwa limekuwa likikiuka haki za wanawake na watoto katika harakati zake za kusaka wakimbizi kutoka kwa kundi la Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Amnesty wanawatuhumu baadhi ya wanajeshi kufanya ukatili wa kingono dhidi ya wanawake katika kambi za wakimbizi wa ndani kama malipo kwa msaada wanaoupatia.

Amnesty inasema kuwa jeshi la serikali katika jimbo la Borno limechafuka,kufuatia kuhusika katika vitendo vya ubakaji na kulazimisha suala la mahusiano na wanawake waliokimbia machafuko.

Riport hiyo ni baada ya mahojiano watu 250 waliohojiwa kati yam waka 2016 na 2018.Makundi ya haki za binadamu yanadai kuwa jeshi wanajinufaisha kimapenzi kwa kutumia mazingira magumu ya chakula yanayowa wakabili wakimbizi hao kisha kuwabaka na kuwalazimisha mapenzi.

Hata hivyo ripoti imeendelea kueleza kuwa wanawake wanadhaniwa walikuwa wake wa wapiganaji wa Boko Haram watano kati yao wamefariki,huku watoto 32 wakidaiwa kufa pia.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amelalamikia ripoti hiyo na kudai kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.