Je majeshi ya Somalia yako tayari kulinda usalama wa nchi hiyo?

Vikosi vya kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM vinatarajiwa kupunguza wanajeshi wa kigeni katika maeneo mbalimbali ya nchini Somalia. Lakini je majeshi ya Somalia yako tayari kulinda usalama wa nchi hiyo?

Mwandishi wa BBC Cyriaque Muhawenayo amezungumza na Tai Gituai, Naibu kamanda wa kikosi cha Amisom mjini Mogadishu.