Wanasayansi Kenya wavumbua dawa ya Malaria kwa waja wazito

Wanasayansi katika taasisi ya utafiti wa afya nchini Kenya KEMRI wanafanyia utafiti dawa mpya ya kuzuia Malaria kwa wanawake waja wazito.

Dawa hiyo, dihydroartemisinin-piperaquine (DP), imefanyiwa majaribio katika maeneo tofauti nchini Kenya ikiwemo, Ahero magharibi mwa nchi, na imegunduliwa kuwa salama kwa matumizi ya kuzuia Malaria kwa wanawake walio na miezi kati ya 4 hadi 9 ya uja uzito.

Ugonjwa wa Malaria una hatari kubwa zaidi kwa wanawake waja wazito.

Miezi mitatu ya kwanza ya uja uzito ndio wakati ambapo watoto wachanga wanakabiliwa na hatari kubwa za athari zinazotokana na dawa za Malaria.

Kesi za malaria kati ya idadi ya watu 1,000, mwaka 2000-2015

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani, ugonjwa wa Malaria unaendelea kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Mnamo 2016, watu 445 000 walifariki kutokana na Malaria duniani ikilinganishwa na 446 000 mnamo 2015.

Watoto walio na chini ya umri wa miaka 5 ndio walio katika hatari zaidi ya kukabiliwa na Malaria.

Maelezo ya picha,

Shirika la Afya duniani inasema watu 4000,000 wafariki kila mwa kwa sababu ya ugonjwa wa malaria

Inakadiriwa kwamba ugonjwa huo husababisha vifo vya watoto wawili kila dakika mbili.

Mambo 10 kuhusu Malaria:

  • Malaria husababishwa na vimelea vinavyosambazwa baada ya mbu walioambukizwa navyo kuwauma binaadamu
  • Takriban nusu ya idadi ya watu duniani wamo katika hatari ya kuugua malaria
  • Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wamo katika hatari kubwa ya kuugua malaria
  • Viwango vya watu wanaokufa kutokana na malaria vinapungua
  • Kutambua na kutibu mapema wagonjwa wanaougua Malaria kunazuia vifo
  • Wasiwasi unaongezeka kuhusu uwezo wa vimelea kupambana na makali ya dawa za kutiba malaria - artemisinin
  • Kulala chini ya vyandarua vilivyotibiwa vya kujikinga na mbu, kunakinga maambukizi ya malaria
  • Kupuliza dawa ndani ya nyumba ndio njia muafaka ya kupunguza haraka maambukizi ya Malaria
  • Wanawake waja wazito ndio wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa malaria
  • Malaria inasababisha athari kubwa kiuchumi katika nchi maskini

Kesi za malaria kati ya idadi ya watu 1,000,katika baadhi ya nchi Afrika, mwaka 2015

Nchi zote kasoro moja zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara - zinashuhudia 80% ya mzigo wa Malaria duniani.

Majaribio yaliofanywa magharibi mwa Kenya katika eneo la Ahero na kwingineko yameonyesha ubora wa dawa hiyo ya DP katika kuzuia Malaria kwa wanawake waja wazito.

Shirika la afya duniani WHO linapendekeza dawa ya Fansidar katika kuzuia malaria miongoni mwa wanawake waja wazito.

Lakini kumeshuhudiwa visa ambavyo ugonjwa unakaidi makali ya dawa hiyo, na kuisababisha kutofanya kazi kwa baadhi ya watu.