Global Newsbeat 24.05.2018: Kutazama runinga muda mrefu huchangia kansa na maradhi ya moyo

Kuketi kwa muda mrefu ukitizama runinga kunachangia kuongeza ugonjwa wa moyo na saratani.

Watafiti katika chuo kikuu cha Glasgow wanasema walipata uhusiano mkubwa kati ya kukaa mda mrefu kuangalia runinga na kudorora kwa afya miongoni mwa watu.

Wasiofanya mazoezi huathirika mara dufu.