Jaji aamuru kijana aliyeng'ang'ania kwa wazazi Marekani aondoke

Michael Rotondo ameamriwa na Mahakama kuondoka nyumbani kwa wazazi wake Haki miliki ya picha CBS
Image caption Michael Rotondo ameamriwa na Mahakama kuondoka nyumbani kwa wazazi wake

Wazazi wawili mjini New York wameshinda kesi waliyokuwa wakipambana kumuondoa kijana wao mwenye umri wa miaka 30 baada ya kukaidi kuondoka

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya juu ya jimboni humo, Jaji aliamuru kijana huyo aondoke nyumbani kwa wazazi wake.

Jaji Donald Greenwood alimwambia kijana huyo kuendelea kubaki nyumbani kwa miezi sita zaidi kama alivyoomba ''haikubaliki''

kijana Michael Rotondo ambaye alijiwakilisha mwenyewe mahakamani, amesema ''Sijui kwa nini hwawezi kusubiri kidogo kabla ya mimi kuondoka,Bwana Rotondo alieleza huku wazazi wakiwa wamekaa karibu na mwanasheria wao wakimtazama.

Alisema kuwa miezi sita ndio muda uli sawa kwa mtu ambaye alikuwa akiwategemea watu .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wazazi wa Michael Christina na Mark Rotondo

Jaji akiwa anatabasamu alimtaka kijana huyo azungumze na wazazi wake,na kuamua kwa hiyari kuondoka nyumbani, lakini Rotondo alikataa.

''Nataka uondoke hapo nyumbani'' Jaji Greenwood aliamuru, kwa mujibu wa kituo cha habari cha ABC

Walipokuwa wakifungua mashtaka juma lililopita,Christina and Mark Rotondo walionyesha nakala ya nyaraka walizokuwa wakimuamuru kuondoka nyumbani tangu tarehe 2 mwezi Februari mwaka 2018.

Sehemu ya nakala zikiwa zimeandikwa ''Kuna kazi zinapatikana hata kwa wale wenye historia mbaya ya kufanya kazi kama wewe'' ''Nenda katafute kazi-unapaswa kufanya kazi!''

Haki miliki ya picha Google maps
Image caption Makazi ya familia ya Rotondo, NewYork

Pia wazazi hao walimpatia dola za Marekani 1,100 ili aondoke nyumbani, kwa mujibu wa barua walimtaka auze baadhi ya vitu vyake ikiwemo gari yake mbovu aina ya Volkswagen Passat.

''Nilitumia na wala sijutii, alieleza waandishi wa habari kuwa alizitumia pesa hizo

Mahakamani Rotondo alikiri kuwa hakuwahi kuchangia gharama zozote nyumbani.

Mahari: Je ni kuchuma mali au kuonyesha shukrani?

Wanawake wanafaa kushinikizwa waolewe?

Baada ya kusikilizwa kwa kesi siku ya Jumanne , Bwana Michael Rotondo aliwaambia waandishi wa habari kuwa atakata rufaa, na amepanga kuondoka nyunbani miezi mitatu ijayo.

Michael Rotondo amesema uhusiano na wazazi wake haujawa mzuri, kiasi cha kutozungumza kabisa ndani ya nyumba.

amesema wazazi wake walimwambia kuwa anaweza kuishi nao miaka minane iliyopita alipopoteza kazi.

Alisema kwa sasa ana kazi , alipoulizwa kuhusu kazi anayofanya alikataa kutoa maelezo zaidi.

Mada zinazohusiana