Wanasayansi Kenya wavumbua dawa ya Malaria ya kutumiwa na waja wazito

Taasisi ya utafiti wa kimatibabu nchini Kenya, KEMRI, imevumbua dawa mpya ya kuwakinga kina mama wajawazito dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

Dawa hiyo inayofahamika kama Dihydro arte-misinin-paiperaquine (DP), ambayo ni tiba mbadala ya ugonjwa wa Malaria inasemekana kuwa salama kutumiwa na kina mama wajawazito.

Uvumbuzi huu una maana gani katika juhudi za kukabiliana na Malaria?

Mtafiti wa KEMRI Dkt Hellen Barsosio anafafanua.