Walter Mong'are: Je, ni kweli kuwa vijana Kenya wanabagua kazi?

Afisa mmoja wa serikali anayeshughulikia maswala ya vijana nchini Kenya Walter Mong'are amekosoa vijana nchini humo kwa kudai wana uvivu wa kutafuta kazi na hubagua kazi.

Walter Mong'are anayesimamia miradi ya vijana katika afisi ya rais amenukuliwa akisema kwamba kazi hazitawatafuta vijana, "Ni lazima utoke nje utafute kazi".

Maoni ya Wakenya ni yepi kuhusu matamshi hayo?