Kiumbe ambaye amewashangaza wataalamu Marekani

Montana Fish, Wildlife and Parks Haki miliki ya picha Montana Fish, Wildlife and Parks
Image caption Kiumbe ambaye amewashangaza wataalamu Marekani

Wataalamu nchini Marekani wameshangazwa na kiumbe mmoja mfano wa mbwa mwitu aliyeuawa na mkulima huko Montana.

Mkulima huyo karibu na mji wa Donton alimpiga risasi kiumbe huyo wiki iliyopita alipokaribia mifugo wake, kwa mujibu wa maafisa.

Wataalamu wa wanyama pori wanasema wameshindwa kutambua ni familia ipi ya wanyama kiumbe huyo anatoka.

Haki miliki ya picha Montana Fish, Wildlife and Parks
Image caption Kiumbe ambaye amewashangaza wataalamu Marekani

Baada ya kumchunguza kiumbe hiyo walisema huenda akawa ni mbwa mwitu kwa sababu meno yake ni mafupi na makucha ni makubwa sana.

"Hatujafahamu hasa huyu mnyama ni wa familia ipi hadi uchunguzi wa DNA ukamilike," msemaji wa shirika ya samaki na wanyamapori alisema.

Alisema itachukua hadi wiki moja kwa matokeo kujulikana, ambayo yatasaidia kumtambua kiumbe huyo.

Haki miliki ya picha Montana Fish, Wildlife and Parks
Image caption Kiumbe ambaye amewashangaza wataalamu Marekani
Haki miliki ya picha Montana Fish, Wildlife and Parks
Image caption Kiumbe ambaye amewashangaza wataalamu Marekani

Mada zinazohusiana