Bilionea Richard Branson ajiandaa kufanya safari ya anga za juu

Chanzo cha picha, Virgin Galactic/MarsScientific.com/Trumbull Stu
Sir Richard atakuwa wa kwanza kusafiri kwa roketi yake SpaceShipTwo
Bilionea Sir Richard Branson anasema anapata mafunzo ya kumwezesha kufanya safari ya anga za juu hivi karibuni.
Aliambia BBC Radio; "Tunazungumza kuhusu miezi kutoka sasa sio miaka, kwa hivyo iko karibu sana. Kuna nyakati nzuri usoni.
"Ninaenda kujifunza kwenda anga za juu ili mwili wangu uweze kujiandaa vyema kwa safari hiyo."
Bilionea huyo wa umri wa miak 67 amekuwa akiwekeza kwa safari za anga za juu tangu mwaka 2004 wakati alianzisha kampuni ya Virgin Galactic.
Sir Richard, mfanyabiashara za teknolojia Elon Musk na mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos sasa wako mbioni kusafirisha abiria wanaolipwa kwenda anga za juu.
Mfanayabiashara huyo raia wa Uingereza alisema; "Elon anafanya vizuri sana kwa kusafirisha mizigo kwenda angani, na anaendelea kujenga roketi kubwa zaidi."

Chanzo cha picha, Blue Origin
Kampuni ya Jeff Bezos Blue Origini ameunda roketi ya kusafirisha watu angani
Lakini upande wa safari za kulipwa ni kati ya Branson na Bezos, mfanyabiashara huyo alisema.
"Nafikiri tuko sako kwa bako kuhusu ni nani atakuwa wa kwanza kusafirisha watu angani, Sie Richard alesema
Sir Richard ana matumaini kuwa atakuwa mtalii wa kwanza kusafiri angani. Alisema mafunzo yake yanaenda vyema na amengeza ubora wake wa mwili kwa kucheza tenisi mara nne kwa siku.
Mapema mwaka huu Virgin Galactic waliakamilisha majaribio ya chombo chake cha SpaceShipTwo ambayo ni roketi ya kusafirisha watu angani.