Matangazo ya vyakula mitandaoni huponza watoto

Vyakula visivyo bora hutangazwa kwenye mitandao ya kijamii ili kuwavutia watoto
Maelezo ya picha,

Vyakula visivyo bora hutangazwa kwenye mitandao ya kijamii ili kuwavutia watoto

Mitandao ya kijamii huenda ikachochea watoto kula vyakula visivyofaa, utafiti umeeleza

Umegundua kuwa watoto wanaojihusisha sana na kutazama mitandao hii wakiona watu wanatumia vyakula vyenye sukari na mafuta kwa wingi nao huiga kwa kula vyakula vyenye asilimia 26% ya vyakula hivyo zaidi kuliko watoto wasiofuatilia mitandao.

Utafiti, uliowasilishwa kwenye Bunge la Ulaya kuhusu unene, ulichambua kuhusu muitikio wa watoto kutokana na picha za mitandaoni.

Matokeo ya utafiti huoyamekuja baada ya kuwepo kwa wito wa kuweka sheria kali dhidi ya matangazo ya vyakula visivyo bora

Nyota wa kwenye mitandao ya kijamii walioainishwa kwenye utafiti ni pamoja na Zoella, mwenye wafuasi milioni 10.9 kwenye mtandao wa Instagram na Alfie Deyes, mwenye wafuasi milioni 4.6.

Watoto 176 waligawanywa kwenye makundi matatu na kuonyeshwa picha za watu maarufu wakitangaza kuhusu vyakula visivyo na afya, vyakula bora, na bidhaa zisizo chakula.

walionyeshwa vyakula vilivyo bora na visivyo bora ili kuchagua, ikiwemo zabibu, karoti, chocolate na pipi za Jeli.

Dokta Emma Boyland, mmoja kati ya watafiti kutoka chuo cha Livepool, akisema kuwa watoto wanaamini watu wanaowaona kwenye picha ni watu kma marafiki zao.

watangazaji hao wamekuwa wakiaminiwa na vijana wadogo hivyo inapaswa watu kuwajibika, Alieleza.

Watafiti wametoa wito wa kuwalinda watoto mitandaoni, hasa kwenye chaneli za mitandao ya kijamii ambako huwa haijulikani kama wanaelewa tofauti kati ya tangazo na maudhui ya kweli.

Maelezo ya picha,

Alfie Deyes ni mmoja wa nyota wa kwenye mitandao ya kijamii aliyetumika kwenye utafiti

Dokta Boyland alisema: ''Kwenye Televisheni kuna maelezo mengi zaidi kuhusu tangazo wakati likiwekwa, kuna muziki ndani ya tangazo na hata mapumziko, lakini kwenye digitali mtazamaji hupewa taarifa nyingi kwa wakati mmoja .

Kiongozi wa jopo la watafiti hao, Anna Coates anasema ''tunajua ukiwaonyesha watoto tangazo la kinywaji, watoto huibuka kukipenda kinywaji hicho.Tulitaka kufahamu mtazamo wao kwa mtu huyu maarufu, kwenye mtandao wa kijamii.

''Tumeona kuwa watoto huvutiwa na watu maarufu mitandaoni , utafiti utakaofuata tutaangalia kama wanaelewa hilo, mara nyingi watu maarufu hulipwa ili kutangaza bidhaa''.

Rais wa Chuo cha afya , kimetaka Serikali kuweka sheria za kumlinda mtoto ambazo zitakuwa mbinu za kupambana na tatizo la uzito mkubwa kwa watoto.