WHO yatoa tahadhari kuhusu watu kuumwa na nyoka
Huwezi kusikiliza tena

WHO yatoa tahadhari kuhusu watu kuumwa na nyoka

Nchi wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia.

Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka.

WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani.

Kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO, kuna nia ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka.

Video: Ferdinand Omondi, BBC

Mada zinazohusiana