Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich apata uraia wa Israel baada ya kuzuiwa Uingereza

Roman Abramovich Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bwn. Abramovich atakua ni mtu tajiri zaidi nchini Israeli

Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya England Roman Abramovich, amesafiri kwa ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata haki ya uraia wa Israel.

Maafisa wa uhamiaji wameiambia BBC kuwa alihojiwa wiki iliyopita kwenye ubalozi wa Israel mjini Moscow. Alikabiliwa na tatizo la kupata upya viza nchini Uingereza katika kinachoonekana kuwa na uhusiano na mzozo wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.

Mzozo huo ulichangiwa zaidi na kupewa sumu kwa jasusi wa zamani na binti wake Sergei na Yulia Skripal.

Msemaji wa Abramovich hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na uraia wake mpya aliopewa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.

Bw Abramovich, mwenye umri wa miaka 51, atakua ndiye mtu tajiri zaidi nchini Israel sasa.

Viza yake ya uwekezaji nchini Uingereza inaripotiwa kuisha muda wake wiki kadhaa zilizopita, lakini serikali ya Uingereza imekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na 'suala lake binafsi'.

Kucheleweshwa kwa utoaji wa viza mpya ya Bw Abramovich kunakuja wakati kukiwa na uhasama wa kiplomasia baina ya serikali za London na Moscow Baada ya kupewa sumu kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal kusini mwa Uingereza.

Bwn Abramovich hakuhudhuria fainali za Kombe la FA katika uwanja wa Wembley mapema mwezi huu wakati Chelsea ilipoichapa Manchester United 1-0.

Vyombo vya habari vya Israeli vinasema kuwa tayari amepewa kitambulisho cha uraia nchini Israeli chini ya sheria ya kurudi nyumbani, ambayo inawawezesha wayahudi popote pale walipo duniani kurudi na kuwa raia wa Israel.

Gazeti la The Times nchini Israeli limeandika kuwa Bw Abramovich aliwasili Israeli Jumatatu na kwamba amehamia nchini humo.

Ni mtu ambaye amekuwa akiitembelea Israeli mara kwa mara na alinunua hoteli mjini Tel Aviv mnamo mwaka 2015 ambayo inasemekana ameigeuza kuwa makazi yake.

Wamiliki wa pasipoti ya Israeli wanaruhusiwa kuingia Uingereza kwa siku chake bila kuwa na visa.

Bw Abramovich ana utajiri wa thamani ya dola bilioni $11.5bn (£8.6bn), kulingana na jarida la Forbes.

Kuhamia kwake Israel kunaweza kumsaidia kifedha kwa sababu kama raia mpya wa Israeli ataweza kuondolewa ushuru unaolipwa na wawekezaji wa kigeni kwa muda wa miaka 10.

Roman Abramovich ni nani?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mr Abramovich (right) has often been spotted at Chelsea's Stamford Bridge ground
  • Ni miongoni mwa watu tajiri zaidi Urusi, aliinunua klabu ya Chelsea FC mwaka 2
  • Inadaiwa aliuza midoli (wanasesere) kabla ya kuwekeza katika mafuta miaka ya 1990 baada ya kusambaratika kwa uliokuwa Muungano wa Usovieti
  • Bw Abramovich alikuwa wakati mmoja mshirika wa kibiashara wa tajiri wa zamani marehemu Boris Berezovky, rafiki wa rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin
  • Wakosoaji wanasema wafanyabiashara hao wawili walitumia ukaribu wao na ikulu ya Kremlin kujipatia umiliki wa mashirika mengi ya serikali kwa 'bei ya kutupa'
  • Bw Abramovich alihudumu kama gavana wa jimbo la Chukotka, Urusi
  • Anaaminika kuwa na urafiki wa karibu na rais wa sasa wa Urusi Vladimir Putin

Unaweza kusoma pia:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii