Je ni mabadiliko gani atakayoleta Dkt Bashiru Ally ndani ya CCM

Dokta Bashiru Ali, Katibu Mkuu wa CCM Haki miliki ya picha Ikulu
Image caption Dokta Bashiru Ali, Katibu Mkuu wa CCM

Kumekuwa na maoni kadha wa kadha kuhusu kuteuliwa kwa Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi, Dokta Bashiru Ally, msomi wengine wakiona kuwa ataweza kuvaa viatu vya Katibu mkuu mstaafu Abdulrahman Kinana.

Wana CCM wana imani CCM Itakuwa mpya kwelikweli wakimtaja kuwa mzalendo wa kweli.

Anaaminika kuwa na umuhimu wa kipekee hata akashika nafasi hii muhimu.

Watu wanaona kuwa kutokana na usomi wake, ni mtu mwenye uelewa mpana wa mambo ikizingatiwa kuwa ni mtaalamu wa sayansi ya siasa.Dokta Bashiru Ally ni nani?

Dokta Bashiru Ally ni mzaliwa wa Mkoa wa Kagera, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Alikuwa mhadhiri katika Idara ya Sayansi ya siasa na utawala, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.

Dokta Bashiru pia ni mkufunzi wa masuala yanayohusu utawala na sheria za ardhi .

Ni mtafiti, na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali.Amekuwa akijihusisha katika shughuli zilizoratibiwa na Taasisi kwa muda mrefu.

Kiitikadi amejipambanua kama mjaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Hapo kabla hakujiweka wazi kama ni mwanachama wa CCM mpaka pale alipoteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati maalumu iliyopewa jukumu la uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi.

Haki miliki ya picha CCM
Image caption Rais Magufuli na Bashiru Ali Katibu Mkuu mpya wa CCM

Kuondoka kwa Kinana ndani ya Chama kulizua maswali kuhusiana na nani ataweza kuvaa viatu vyake, na hasa baada ya kurejea kazi alizozifanya za kisiasa kwani Kinana aliongoza kampeni za rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, na kusimamia kazi mbali mbali za utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Falsafa yake ya kijamaa, imejenga wasifu wa nje wa Kinana unaoakisi kusimamia kile alichokiamini ndani ya chama chake,huku akitajwa kubobea katika uenezi na ambaye amepata mafunzo katika nchi mbali mbali za kikomunisti jambo ambalo linazidisha kuendelea kuhitajika kwake hata alipoamua kustaafu.

Hata hivyo katika shughuli za ujenzi wa chama akiwa katibu mkuu wa chama , Kinana alizunguka nchi nzima kufanya shughuli mbali mbali za chama akishirikiana na watu katika kazi za mikono na kula nao chakula jambo ambalo linatajwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa kwamba lilikiimarisha zaidi chama hicho na kuongeza mshikamano.

Haki miliki ya picha CCM
Image caption Wajumbe wa CCM katika mkutano wa siku mbili uliomalizika jijini Dar es Salaam.

Ni mtu ambaye amekuwa akiiamini na kuitekeleza falsafa ya kijamaa,haiba yake ikionyesha uwezo wa kujenga umoja na kuunganisha watu ndani ya chama chake,kuondoka kwake kuna acha swali kwamba je ni nani baada yake atakayevaa viatu vyake,hilo ni jambo la kusubiria moshi mweupe kutoka ndani ya kikao cha halmashauri kuu ya chama taifa ambacho kimeendelea kwa siku ya pili leo.

Abdulrahman Kinana ni nani?

  • Abdulrahman Kinana alizaliwa miaka 66 iliyopita Arusha, Kaskazini mwa Tanzania
  • Kinana ni mwanasiasa nguli aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini.
  • Alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani akibobea kwenye masuala ya mikakati
  • Alikuwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimatafa na Waziri wa ulinzi.
  • Kinana aliwahi kufanya kazi na Jeshi la wananchi la Tanzania kwa miaka 20 kabla ya kusaafu akiwa na cheo cha ukanali mwaka 1972.
  • Abdulrahman Kinana pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006.

Ni mwanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alikuwa mstari wa mbele katika kampeni za urais kuanzia mwaka 1995 wakati Rais Benjamini Mkapa alipokuwa katika harakati za kuwania urais halikadhalika katika kipindi cha Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Abdulrahaman Kinana

Kinana aliwahi kuwa mwakilishi wa diplomasia wa rais wa Tanzania katika eneo la maziwa makuu na kabla ya hapo alikuwa mwenyekiti wa mawaziri wa ulinzi wa nchi za kusini mwa Afrika, SADC wakati huo akiwa Waziri wa ulinzi katika serikali ya Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii